Kilele Cha Furaha Yetu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Kilele Cha Furaha Yetu
Loading
/
I Wakorintho 15:51-58

Hujambo na Karibu.

Leo twalichambua neno la Mungu pamoja kutoka 1 wakorintho 15: 51-58, KILELE CHA FURAHA YETU. Jina langu ni David Mungai, wimbo halafu tuendelee.


naam, karibu tena tujifunze neno la Mungu pamoja Katika Biblia 1 Wakorintho 15:51-58, KILELE CHA FURAHA YETU

Twapata maneno yanayofundisha kwamba siku itafika amabyo furaha yetu itafikia kilele chake cha milele wakati huo tutaona ahadi zake Mungu zikitimia. Yale yote Mungu ametuahidi yatatimia tupende tusipende

Kristo yu hai, na alifufuka kama alivyokua amesema na kuahidi. Ahadi zake ni kweli. Nasoma sasa 1 Wakorintho 15: 51-58, KILELE CHA FURAHA YETU

Ndugu zangu nisemavyo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithui ufalme wa Mungu wala uharibifu kurithi kutokuharibika

51 Angalieni nawaambia ninyi siri hatutalala sote ninyi siri, hatutalala sote, lakini sote tutabadilika

52 Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho maana parapanda italia na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasi tutabadilika

53 Maana sharti meili huu uharibikao uvae kutokuharibika nao huu wa kufa uvae kutokufa

54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika na huu wa kufa utakapovaa kutokufa hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa mauti imemezwa kwa kushinda

55 ku wapi ewe mauti kushinda kwako? U wapi ewe, mauti uchungu wako?

56 Uchungu w amauti ni dhambi na nguvu za dhambi ni torati

57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa bwana wetu Yesu Kristo.

58 Basi ndugu zangu wapendwa mwimarike msitikisike mkazidi sana kutenda kazi ya bwana siku zote kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika bwana

Katika fungu hili la neno la Mungu Pauklo, ajibu swali hili. Je itakuwaje kwa wale wasiokufa? Paulo asema hivi katika mstari wa 51

“angalieni nawaambia ninyi siri hatutalala sote lakini sote tutabadilika”

Kristo arudipo kunao wale watakuwa bado hai lakini miili yetu itabadilishwa na kupewa miili ya utukufu.

Pia Paulo awatia moyo kuhusu ukweli huo kwa maneno haya

1 wathes 4:15 kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la bwana kwamba sisi tulio hai tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake bwana hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti

Bwana wetu Yesu Kristo akirudi sasa hivi kulinyakua kanisa lake waliokufa katika Yesu Kristo watafufuliwa kwanza na sote tunyakuliwe kwenda angani baada ya hiyo dhiki ya miaka saba itaanza wanaomwaamini Yesu hawataingia katika dhiki maana tutakuwa na Yesu angani. Katika dhiki maana tutakuwa na yesu angani. Katika miaka saba ya dhiki watakaokataa kumwabudu mpinga Kristo watauawa lakini mwishoni mwa wakati wa wataofufuliwa nasi turudi na kristo duniani hii na sote tuingie katika ufalme wake Yesu wa miaka elfu moja.

Na ukweli huu hututia nguvu katika huduma yake bwana Yesu kama tunavyosoma katika mstari wa 58

1 wakori 15:58

Basi ndugu zangu wapendwa mwimarike msitikisike mkadizi sana kutenda kazi ya bwana siku zote kwa kuwa mwajia ya kwamba taabu yenu siyo bure katika bwana.

Msikilizaji mpenzi jipe nguvu katiak Yesu Kristo taabu unayopitia si ya bure. Utazawadiwa na Mungu

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!