Masalaba Hugawanya

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Masalaba Hugawanya
Loading
/
I Wakorintho 1:18-25

Hujambo. Karibu tujifunze Neno pamoja. Hiki ni kipindi cha “MATUMAINI.” Leo twakitazama kifungu cha Neno kutoka 1 Wakor. 1:18-25. “MSALABA HUGAWAANYA.” Wimbo halafu tuendelee.

Wimbo

Naam. Karibu tena. Twalichambua fungu la Neno la Mungu, kutoka 1 Wakor. 1: 18-25.

Mfume Paulo alipotoa hotuba yake pale mlimani wa Mass Hill, alisema.

Matendo 17:24-27

24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa mbingu nan chi , hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono.

25 Wala hatumikwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote, kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wan chi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuvu tangu zamani na mipaka ya makazi yao.

27 Ili wamtafute Mungu ingawa ni kwa kupapasa-papapsa wakwmwone ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.

Kwa kifupi: hakuna mtu anayeweza kusimama na kujigamba alivyo mkamilifu bila msalaba wa Yesu.

Msalaba wa Yesu hutugawa, watu wa kwenda mbinguni na wengine na kuachwa nyuma. Ujumbe wa msalaba ni wa unyenyekevu, maana bila kifo cha Yesu msalabani hatuwezi kuoshwa na dhambi zetu.

Anayetubu na kumwamini Yesu husamehewa na dhambi zote.

Anayekataa, bado amefungwa na dhambi zake na hukumu ya kifo yamlalia. Waona, msalaba umetugawa. Lazima tujifunze kunyenyekevu.

Nasoma sasa fungu letu la leo. 1 Wakor. 1:18-25:

18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu ya Mungu. Ligi kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili, nitazikataa.

20 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja ya zamani hizi? Je! Mungu hakulifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?

21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata, kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno liliohubiriwa.

22 Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima.

23 bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesubuliwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayahudi ni upuzi

24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.

25 Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

26 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu ya kwamba, si wengi wenye hekima ya mwili, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa,

27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviabishe vyenye nguvu.”

Msalaba wa Yesu, wahimiza wito. Witio wa kuamua, kwa unyenyekevu, kujitoa kwake Yesu. Kwamua kwa moyo wa dhati, bila kufikiria kurudi nyuma. Kuangalia mbele na macho ya kiroho, kama Jeshi la wokovu. Msalaba wa Yesu huleta mgawanyiko au utengano.

Katika mstari wa 18 1 Wakor: 18, “ Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu ya Mungu.”

Kwa kifupi, maneno hayo yasema: “Ni uokolewe upate nguvu ya Mungu au ubaki katika njia ya upotevu.” Kwisha.

Na katika mstari wa 19, twasoma, “Kwa kuwa imeandikwa, nitaiharibu hekima yao wenye hekima. Na akili zao wenye akili nitazikataa.

Yaani, ni uokee hekima ya Mungu, kwa Imani, au uache kwa sababu kwa akili zako huendi popote.

Mtu mmoja William Barclay, alijaribu kuthibitisha ya kuwa Yesu hakufufuka lakini mwisho wa uchanguzi wake, aliamini kwamba, Yesu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu, na akamwamini Yesu.

Msalaba wa Yesu uliharibu hekima zote za ulimwengu. Ni kwa Imani tu katika Yesu, twaweza kujitwalia wokovu na uzima wa milele.

Katika mst 24 na 25, twasoma:
“bali kwao waitwaoo Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo nguvu ya Mungu , na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu. Watu wengi hutawaliwa na kiburi na kudhani ya kuwa wao ni bidhaa adimu.

Kwa kifupi ni kusema: Ni umwombe Mungu akupe nguvu za ushindi maishani au utaendelea kusumbuka bure ukidhani utapata Amani rohoni na moyoni mwako.

Ni aidha uyafuate ya kiroho katika Kristo au, uyazingatie ya dunia, tamaa za kimwili na dunia, zinzaoelekea kuzimu, au uyapokee ya msalaba wa Yesu upate wokovu na uzima wa milele.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!