Makao Yetu Mbinguni

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Makao Yetu Mbinguni
Loading
/
II Wakorintho 5:1-10

Natumai u buheri wa afya, msikilizaji mpenzi.

Karibu tujifunze neno pamoja, 2 Wakorintho 5:1-10

‘MAKAO YETU MBIGUNI’

Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tundelee.

Naaam na kaributuendelee kujifunza neon. Leo twalichabua funghu la neno kutoka 2 Wakorintho 5:1-10. Makao yetu mbinguni. Nasoma fungu hili:

1 Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.

2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;

3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.

4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.

5 Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho.

6 Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.

7 Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.

8 Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.

9 Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.

10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. Kutoka kwa fungu hili la Neno twapata mafunzo kadhaa.

I. Mstari wa 5-7. Twapata uhakika wa Paulo, kwamba, tunapokuwa katika hali ya kukaa raha mstarehe, kimwili na katika mambo ya dunia, ni rahisi sana kuwa mbali na Mungu.

Sababu ni kwamba, ya dunia ni hafifu yakilinganishwa na ya mbinguni, na yale tutakaotunukiwa Kristo arudipo. Mstari wa 6.‘Basi siku zote tuna moyo mkuu, tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili,tunakaa mbali na Bwana((7) maana twaenenda kwa Imani, si kwa kuona.’

8 Lakini tuna moyo mkuu, nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. Twahitaji kumpendeza Bwana.

2 Katika mstari wa 9 mwisho…twajitahidi kumpende zayeye.

Lengo la Paulo,lilikuwa kumpendeza, Kristo, katika maisha yake ili Kristo arudipo ambadilishe mwili, na kumpa mwili wa utukufu, mwili wa kimbinguni, mwili ambao hauji maradhi wala kifo. Na hilo ndilo lengo letu sote tunayemwamini Yesu Kristo na kumpokea kuwa mwokozi wetu.

Jipe moyo ndugu/dada Mkristo, siku yaja ambayo hayo yote tunayotaraji katika Yesu yatatimia.
Mungu mwenyewe atayatimiza kikamilifu.

3 Katika mstari wa 10 twapata maneno haya:

‘kwa maana imetupasa sisi sote kuthihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.

1 Wote wanaompenda Yesu tutapewa Taji la haki 2 Tim 4:8

2 Wanaowaleta watu kwa Kristo, watapewa taji 1 Wakor 2:19

3 Wampendao Yesu wote wapewa taji la uzima.

4 Wachungaji wa wanaomwamini Yesu watapewa taji la utukufu.I Peter 5:4

5 Wanaoteswa kwa sababu ya Imani yao,watapewa taji la uzima. Ufunuo 2:10

Kwa Imani hayo yote ni yetu katika Kristo Bwana. Jipe moyo ndugu au dada Mristo. Mateso, masumbuko,ni ya muda mfupi. Waraka wa Paulo14:10-11,neno lasema:

‘Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako?

Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu. Kwa kuwa imeandikwa kama niishivyo, anena Bwana,kila goti litapigwa mbele zangu, na kila ulimi utamkiri Mungu.

Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbeleza Mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!