Utumishi Wake Paulo Kwa Wakorintho

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Utumishi Wake Paulo Kwa Wakorintho
/
II Wakorintho 12:11-18

Hujambo msikilizaji na karibu tujifunze neon pamoja. Leo twalichambua fungu la neon kutoka 2 Wakorintho 12:11-18 Utumishi wake Paulo kwa wakorintho. Jina langu ni David Mungai karibu wimbo alafu tuendelee

Naam karibu tena tujifunze neon 2 Wakorintho12:11-18 utumishi wake Paulo kwa wakorintho nasoma fungu hili la neon

11 Nimekuwa mtu asiye na akili. Ninyi mlinilazimisha kuwa hivyo, kwa maana ninyi mlipaswa kunipendekeza. Kwa maana hata katika jambo moja sikuwa mdogo kwa mitume wenu walio bora sana, hata kama mimi si kitu.

12 Kwa kweli, ishara za mtume zilitokezwa katikati yenu kwa uvumilivu wote, na kwa ishara na mambo ya ajabu na matendo yenye nguvu.

13 Kwa maana ni katika jambo gani kwamba ninyi mlikuwa wadogo kuliko yale makutaniko mengine, isipokuwa kwamba mimi mwenyewe sikuwa mzigo kwenu? Mnisamehe kosa hili kwa fadhili.

14 Tazama! Hii ndiyo mara ya tatu niliyo tayari kuja kwenu, na bado sitakuwa mzigo. Kwa maana ninatafuta, si mali zenu, bali ninyi; kwa maana watoto hawapaswi kuweka akiba kwa ajili ya wazazi wao, bali wazazi kwa ajili ya watoto wao.

15 Kwa upande wangu mimi nitatumia kwa furaha zaidi na kutumiwa kabisa kwa ajili ya nafsi zenu. Kama nikiwapenda ninyi kwa wingi zaidi, je, mimi nipendwe kidogo?

16 Lakini hata iweje, mimi sikuwa mzigo mzito kwenu. Hata hivyo ninyi mnasema, mimi nilikuwa “mjanja” nami niliwashika ninyi “kwa ujanja.”

17 Kwa habari ya yeyote kati ya wale niliowatuma kwenu, je, niliwatumia ninyi kwa kujifaidi kupitia yeye?

18 Nilimhimiza Tito na nikamtuma yule ndugu pamoja naye. Je, Tito aliwatumia ninyi kwa kujifaidi hata kidogo? Je, hatukutembea katika roho ileile? Katika hatua zilezile?

Kutoka kwa fungu hili la neon, Paulo atoa vile utumishi wake kwa wakorintho ulivyokuwa. Kwanza kabisa katika mstari wa kumi na mmojaaonyesha kuwa hakuwa duni na watume waliokuwa kati ya wakorintho kimzaha awaita waalimu wa uongo. Mitume walio wakuu Paulo alijitaja kuwa mdogo wa mitume maana awali alilitesa kanisa akasema ni kuwa neema yake mungu akaitwa na mwenyezi

Mungu kuwa mtume. Na ishara za mtume wa kweli zaonyeshwa kwa kuokolewa kwa mtu kutoka dhambini na kumfanya awe kiumbe kipya n ahata matendo. Tukijua ya kwamba mtu mabalozi wake duniani hii. Ishara ya wokovu Zaidi ishara za sarakasi.

Sarakasi ni za hapa hapa tu lakini uzima wa milele na milele amina.

Maneno ya mstari wa 14-15 twaona ya kwamba Paulo ajitayarisha kutembelea kanisa la korintho akitarajia kuona mabadiliko haswa ya kiroho kwa sakorintho. Paulo ndiye alilianzisha kanisa hilo akalitembeleasafari ya pili lakini akahuzunikshw sana na tabia zao akwapelekea waraka wa pili mkali sana lakini ukapotea sasa hapa awaambia kwamba apanga namna ya kuwatembelea dhambi huleta hasara kimwili, akili n ahata kiroho. Mtume Paulo, atamani sana kuwatembelea mara ya tatu apate kuwasaidia kuwatembelea wakristo wenzake husaidia kukua kiroho pamoja na hayo.

Unawapowatembelea wakristo wenzako mtashirikiana katika kulisma neon, kuomba n ahata kumsifu mungu.

Wakorintho, kama binadamu wengine husababisha kutoaminiana. Kanisa la korintho lilichabga pesa za msaada kupelekea kanisa la yerusalemu walizingizia kwamba hawakujua yote yaliyohusu zile pesa. Paulo aliwaomba watubu waungame kwa sababu hakuingusa ile fedha

Na kwa Ushahidi wa kutosha. Tusiyaseme tusiyoyajua bali tuizingatie yaliyo kweli. Na kweli itadumu na hayo hudumisha Imani.