Maono Yake Paulo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Maono Yake Paulo
Loading
/
II Wakorintho 12:1-10

Hujambo na karibu. Leo twalichambua neon la mungu kutoka kitabu cha 2 Wakorintho12:1-10, MAONO YAKE PAULO. Jina langu ni David Mungai. Wimbo alafu tuendelee.

Naam karibu tena tujifunze neon pamoja. 2 Wakorintho 12:1-10. Maono yake Paulo, Jina langu ni David mungai. Nasoma fungu hili la neon

1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kupitia mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu kwa kutaniko la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu+ wote walio katika Akaya yote:

2 Na muwe na fadhili zisizostahiliwa na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

3 Abarikiwe Mungu na Baba ya Bwana wetu Yesu Kristo, Baba ya rehema nyororo na Mungu wa faraja yote,

4 ambaye hutufariji katika dhiki yetu yote, ili tuweze kuwafariji wale walio katika namna yoyote ya dhiki kupitia faraja ambayo sisi wenyewe tunafarijiwa na Mungu.

5 Kwa maana kama vile mateso kwa ajili ya Kristo yalivyo mengi katika sisi, vivyo hivyo faraja tunayopata pia ni nyingi kupitia Kristo.

6 Basi kama tumo katika dhiki, hiyo ni kwa ajili ya faraja na wokovu+ wenu; au kama tunafarijiwa, hiyo ni kwa ajili ya faraja yenu inayotenda ili kuwafanya mvumilie mateso yaleyale ambayo sisi pia tunateseka.

7 Na kwa hiyo tumaini letu kwa ajili yenu haliyumbi-yumbi, tukijua kama tunavyojua kwamba, kama vile mlivyo washiriki wa hayo mateso, vivyo hivyo ninyi pia mtaishiriki faraja.

8 Kwa maana sisi hatutaki ninyi mkose kujua, akina ndugu, juu ya dhiki iliyotupata katika wilaya ya Asia, kwamba tulikuwa chini ya mkazo mkubwa mno unaoshinda nguvu zetu, hivi kwamba hatukuwa na uhakika kabisa hata juu ya uhai wetu.

9 Kwa kweli, tuliona ndani yetu wenyewe kwamba tumepokea hukumu ya kifo. Ilikuwa hivyo ili uhakika+ wetu uwe, si katika sisi wenyewe, bali katika Mungu ambaye huwafufua wafu.

10 Kutoka katika kitu kikubwa sana kama kifo alituokoa naye atatuokoa;+ na tumaini letu limo katika yeye kwamba atatuokoa zaidi pia.

Katika fungu hili la neon, Paulo anazungumzia ule wakati alinyakuliwa mpaka mbingu ya tatu, akafunuliwa mafunuo ambayo hangeweza kueleza. Baadhi ya wasomi hufikiria kwamba Paulo alinyakuliwa wakati wa kupigwa kwake kwa mawe kama tunavyo soma katika matendo ya mitume 14:19

Baada ya hayo katika mstari wa 7 twaona ya kwamba Paulo alipewa mwiba katikamaisha yake asije akajivuna eti yeye alikuwa amenyakuliwa moaka mbingu ya tatu

Baadhi ya wasomi husema ya kwamba labda Paulo aliumwa na kichwa mfululizo, wengine husema ilikuwa shida ya macho wenginemalaria, wngine kifafa, lakini twaamini ulikuwa mwiba wa kumtuliza Pulo asije akajivuna kupita kiasi. Mwnyewe Paulo aliona ule mwiba kanakwamba ulikuwa kazi ya shetani lakini Mungu aliruhusu asijivune. Mungu hakumchukia kiburi. Mungu hupendezwa nasi tunapomtegemea yeye pekeyake. Hata taifa la Israeli, taifa teule lilipotafuta msaada kutoka kwa mataifa mengine, mungu aliwaletea maradhi na misukosuko. Hatupaswi kumlinganisha mung una kitu kingine chochote. Hakuna Mungu kama Mungu wetu katika Kristo, Hkuna!

Paulo alimwomba mungu amwondolee ule mwiba lakini Mungu akamwambia Pulo kwamba neema yake mungu yatosha

Hayo yote yatupata; mabo yet una yawe, neema ya mungu iwe pamoja nasi na tunapokuwa wadhaifu, nguvu na uweza wa kristo ziwe pamoja na kila mmoja kwa neema yake

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!