Kanisa La Kweli

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Kanisa La Kweli
Loading
/
I Wakorintho 14:34-40

Hujambo msikilizaji wangu popote ulipo. Karibu ujifunze neno pamoja. 1 Wakorintho 14:34-40. Kanisa la kweli jina langu ni david mungai, karibu wimbo

Ni wimbo mtamu. Sasa tuendeleekujifunza neno. Kanisala kweli.

Mtu mmoja alisema hakuna kanisa au dhahebu kamilifu na hii ndiyo sababu sijajiunga na lolote. Mkristo rafiki yake akaamwambia utakalipata kanisa au dhehebu lisilo na kosa, usijiunge nalo maana duniani hii hakuna. Rafiki mwenzake aliendelea kumwambia ukilipata kanisa lililo kamilifu usijiunge nalo wewe mwenyewe maana utaliharibu.

Ukweli halisi ni kwamba hakuna dhehebu au kanisa lisilo na waa. Katika 1 wakorintho 14:34-40 paulo atuonyesha mfano wa kanisa lililo sawa- kamilifu nasoma sura hiyo

34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa maana hawana ruhusa kunena bali watii kama vile inenavyo torati nayo.

35 nao wakitaka kujifunza neno lolote na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa

36 au je! Neno la mungu lilitoka kwenu ? au kuwafikia ninyi peke yenu?

37 mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni na ayatambue hayo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya bwana

38 lakini mtu akiwa mjinga na awe mjinga

39 kwa ajili ya hayo ndugu takeni sana kuhutubu wala msizuie kunena kwa lugha

40 lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu

Uzuri na utaratibu ni mambo muhimu katika kanisa na mkutano inayohusu kanisa.

Katika kanisa la mungu lazima liwe na uzuri wa kutamanika na utaratibu wa ungwana. Zamani niliwaona wazazi wangu walikuwa macho katika mambo yaliyohusu kanisa. Walikuwa na nguo za kuhudhuria ibada n ahata shughuli zingine za kanisa. Hata wakiwa katika eneo la kanisa walitulia tuli, ni tofauti sana na siku hizi. Kanisa husimamia uwepo wake mungu na mungu hawezi kuchanganywa na mengine
Mavazi na sauti ya viatu na mazungumzo hata masengenyo ndani ya kanisa mavazi ya dada zetu wacha tu.

Neno lasema kumbukumbu la torati 6:4-6

Sikiza ee Israeli, bwana munu wetu, bwana ndiye mmoja.

Nawe mpende bwana mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote

Na maneno haya ninayokuamuru leo yatakuwa katika moyo wako.

Moyo wa mtu ndiyo engine ya mambo yote anayofanya na hivi ukimwachia mungu atawale moyo wako.

Basi na matendo yako kanisani na popote pale yatakuwa kulingana na mapenzi ya mungu.

Pamoja na hayo twahitaji neema kanisani mwake mungu

Mst36-38

‘Au je! Neno la mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?

Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni na ayatambue hayo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya bwana lakini mfu akiwa mjinga na awe mjinga.’

Katika maneno ya mtaari wa6 paulo awaulize washiriki wa kanisa la korintho Je, neno lilitoka kwenu?
Neno tunalolisikia kanisani ni ujumbe kutoka kwa mungu, ni ujumbe wa roho na dhamiri zetu. Ni lazima ulisikilize kwa makini tuache dhihaka na utani

Tukae kimya tupakuliwe kwa heshima zote na kwa utukufu wake mungu. Neno lake ndilo nguvu zetu na taa yetu ya maisha haya

Mungu husema nasi kwa neno lake kama vile na hii ndiyo sababu sisi husoma maneno haya. Mungu amesema na kurudiwa mara 3,500 katika biblia kwa hiyo wakati wa ibada tuliheshimu neno kwa sababu ni sauti yake

Mungu amewasiliana nasi kinaga ubaga kwa maumbile yake, mbingu na nchi humtolea mungu utukufu. Mwanadamu apaswa vivyo hivyo

Katika ibada zetu kusiwe mahali mabishano bali kwa utulivu na utaratibu maalum tumpe mungu heshima zetu zote, kila mtu afanye sehemu au kazi yake kwa ustadi na tutabarikiwa.

Neno korintho halitoi maana jema- maana yake ni kile kati ya mwanaume na mwanamke lakini walikuwa kanisani na kwa neema yake aliwabadilisha kwa neema

Bwana mungu sisi pia kwa neema yako tujalie na utusamehe dhambi utufanye viumbe viteule kanisani na popote tuwapo kwa utukufu wako tuneemeshe twakuomba katika jina tukufu la yesu, amen

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!