Ibada Kwa Wote

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Ibada Kwa Wote
Loading
/
I Wakorintho 14:23-33

Hujambo na Karibu.

Leo twalichambua fungu la Neno kutoka 1 Wakorintho 14:23-33 ‘ IBADA KWA WOTE’ Jina langu ni David Mungai wimbo halafu tuendelee.

Karibu tena msikilizaji, wakati wa shida wangu/ watu huongezeka katika ibada makanisani haswa wakati wa mateso ya wanaomwamini Yesu. Zaidi sana wakristo walipigania Imani, miaka ya 1500, mpaka 1600 AD. Wakristo wakaanza kukutana katika vikundi vidogo vidogo kisiri, wakijificha. Hata hivyo sharti tujue, kanisa ni la wote wanaomwamini Yesu na wameitwa watoke waeneze Injili. Tumeitwa tujitokeze kwa huduma mbalimbali Lakini ni muhimu kukutana mara nyingi iwezekanavyo, kutiana nguvu katika ushirika wa undugu kama tunavyosoma katika Waebrania 10:23-25
23 na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke, maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu,

24 tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri,

25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine bali tuonyane, na kuzidi kufanya hivyo kwa kadri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.”

Ni muhimu kukusanyika katika umoja wa Imani yetu katika Bwana. Kama ilivyofanya kanisa la kwanza katika matendo ya mitume.

Nasoma sasa kutoka 1 Wakorintho 14:23-33
23 Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha , kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, Je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?

24 Lakini wote wakihutubu kisha akaingia mtu asiyeamini au mjingi, abainishwa na wote, ahukumiwa na wote,

25 siri za moyo wake huwa wazi, na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudifudi, na kukiri ya kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka,

26 Basi ndugu, imekuaje? Mkutanoni pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo. Ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa Kusudi la kujengwa,

27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu na mmoja afasiri.

28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa, aseme na nafsi yake tena na Mungu.

29 Na manabii wanene wawili au watatu, na wengine wapambanue.

30 Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze,

31 kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wafarijiwe,

32 Na roho za manabii huwatii manabii

33 kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali wa amani vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu

Katika na ndani ya ibada, sharti na lazima pawe na mawasiliano la sivyo ibada itakuwa si ibada mahali pa kumwabudu mwenyezi Mungu.

Katika Ibada, twawasiliana na Mungu, na pamoja humsifu na kumtukuza Mungu, na kiroho tupate kujengana tukue, tuimarike kiimani.

Jambo la pili, ni muhimu tuchukuliane na kuitiana nguvu, kwa shuhuda zetu na kushirikiana katika changamoto maishani.

Ukurasa 26-28 “Basi ndugu imekuaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana saburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tfsiri. Mambo yote na yatendeke kwa Kusudi la kujenga.

kama mtu akinena kwa lugha , wanene wawili , watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu na mmoja na afasiri.

Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa, aseme na nafsi yake tena na Mungu.

Mawasiliano, yanayoeleweka katika kanisa ni muhimu sana. Wenye kuhutubu wahutubu kwa njia inayoeleweka na manabii wanene wawili, na watatu, na wengine wapambanue.

Tukumbuke ya kwamba ibada yaweza kuchukua muda mwingi, Lakini lazima mawasiliano yawe safi kwa sababu twaweza kuwakwaza wengine wasielewe na ukweli wa Neno.

Katika ibada ya watu wote, basi tuchukuliane, na tuheshimu na tumwabudu Mwenyezi Mungu na kwa heshima za mwenyezi Mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!