JINSI YA KUHESABIWA HAKI MBELE ZA MUNGU

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
JINSI YA KUHESABIWA HAKI MBELE ZA MUNGU
Loading
/

MATUMAINI PROG 1499
TITLE: JINSI YA KUHESABIWA HAKI MBELE ZA MUNGU
TEXT: WAGALATIA 2:15-19
Hujambo na karibu popote ulipo leo twalichambua neno kutoka waraka wa Paulo kwa wagalatia 2:15-19 jinsi ya kuhesabiwa haki Mbele za mungu. jina langu ni David Mungai, karibu wimbo alafu tuendelee
WIMBO
Naam karibu tena twalichambua fungu la neno la mungu kutoka waraka wa Paulo kwa wagalatia 2:15-19 jinsi ya kuhesabiwa haki Mbele za mungu
Ni jambo la haki kuwa ndani ya kila mmoja wetu, tunacho kiu na njaa ya kumjua mungu Zaidi twapenda kujua namna ya kuhesabiwa haki maana tulizaliwa katika dhambi na kwa kweli dhambi imetutesa sana
Nasoma fungu hili la neno wagalatia 2:15-19

15 Sisi tulio Wayahudi wa kuzaliwa na sio watu wa mataifa ‘wenye dhambi,’16 tunafahamu kwamba mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa kutii sheria bali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa kumwa mini Kristo, na wala si kwa kuitii sheria. Maana hakuna mtu ata kayehesabiwa haki kwa kutii sheria. 17 Lakini ikiwa sisi katika jitihada ya kuhesabiwa haki katika Kristo, bado tunaonekana tun gali wenye dhambi, je, hii ina maana kwamba Kristo amekuwa mwene zaji wa dhambi? La hasha! 18 Lakini ikiwa mimi nina jenga tena kile ambacho nimekwisha bomoa, basi ninadhihirisha kwamba mimi ni mvunja sheria. 19 Kwa maana mimi kwa njia ya sheria, nimeifia sheria, ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu.

Fungu hili la neno la mungu latuonyesha yakwamba ili tuhesabiwe haki twapaswa kuchukua hatua angaa tatu
1 lazima tuelewe msingi. Msingi huo ni yesu kristo nasoma tena mstari wa 19
Maana mimi kwa njia ya sharia niliifia sharia ili ni mwishie mungu
Msingu wa kuhesabiwa haki kwetu ni kumwamini na kumwishia yesu kristo. Palo akiwaandikia warumi alisema, kwamaana sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa mungu ni yesu kristo tu bwana wetu ambaye hakutenda lakini alisulubiwa msakabani awe fidia yea dhambi zetu. Yesu tu ndiye anayefaulu kuwa msingi wa kuhesabiwa haki kwetu
2 hatua ya pili ya kuhesabiwa haki kwetu ni kwamba lazima tujifunze kuuliza swali hili, yesu kriso yu wapi katika jambo hili? Sisi twahesabiwa haki kwa kumwamini Yrsu kristo kwa sababu ni yeye mpatanishi kati yetu na Mungu. nasoma mstari wa 17
Lakini ikiwa sisi wenyewe kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika kristo tulionekana kuwa wenye ndhambi je kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha!
Ndiyo tumepatikanan kuwa wenye ndambi lakini ni katiak kristo sisi kuhesabiwa haki yesu kristo ndiye njia yetu ya kuhesabiwa haki
Hatua ya tatu lazima tujue na kuamini ni katika yesu kristo sisi huwekwa huru kuwekwa huru ni hatari sana tusipowajibika kuishi maisha yetu katika yesu kristo kwa kanuni na kweli za neno lake mungu twaweza kuhesabiwa haki.
Lazima tuwe na uhusiano wa kudumu, lazima pawe na mawasiliano. Mawasiliano yetu na mungu ni kupitia kwa yesu kristo, kuomba kumwabudu mungu na kumpa nadasi ya kwanza maishani kwetu. Ni yeye tu tunaweza kuabudu. Je wajua ya kwamba ni yesu kristo bwana wetu tutaishi kuabudu.
Naomba kwamba roo mtakatifu awe nguzo kaktia mioyo na katika matendo yako

OMBI
Endapo wahitaji msaada Zaidi, tafadhali wasiliana nasi. Anwani na nambari za simu ntazisomna baada ya wimbo huu
WIMBO
MATUMAINI
TWR
SLP 21514-00505
NAIROBI KENYA
SIMU: 0721970520
BAURA PEPE: [email protected]
Jina langu ni david mungai, kwaheri kwa sasa.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!