Wagalatia 3:15-18
Hujambo msikilizaji wangu karibu sana tujifunze neno la mungu, leo twajifunza kwa undani fungu la neno nkutoka warakawa Paulo kwa Wagalatia 3:15-18, jina langu ni David mungai, wimbo alafu tuendlee
Naam katibu tena tujifunze neno, Wagalatia 3:15-18 ukweli wa agano na ibrahimu
Baba yetu ibrahimu ni mtu muhimu na wa maana katika mpango wa mungu kwetu na katika hitoria inayoonyesha namna mungu alidumisha uwepo wake kwa ibrahimu ni muhumu na tunayo sababu ya kujua na kufahamu ukweli wa agano katia ya mungu na ibrahimu. Hata yesu mwenyewe aliyazungumzia hayo katika vitabu vya injili.
Mtume Paulo pia aliwakumbusha wakorinho na warumi kuhusuagano hili sasa nasoma waraka wa Paulo kwa Wagalatia 3:15-18
15 Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno.
16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.
17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi.
18 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Ibrahimu kwa njia ya ahadi.
Katika fungu hili la neno tunayo maneno Fulani yanayoonhyesha wazi ukweli halisi wa ahadi hii
Agano au makubaliano kati ya wawilihuonekana ahadi iliyopo ukitimia
Miaka mingi iliyo tangulia na kupita mungu aliwaahidi ibrahimubaraka kwa maneno haya, mwanzo12: 3
Name nitawabariki wakubariki naye akulaaniye nitamlaani na katika wewe jamaa zote zadunia watabarikiwa
Na katika mwanzo 17:4-5
Mimi agano langu nimefanya nawe nawe utakuwa baba wa mataifa mengi
Wala jina lako hutaitwa tena. Abrahamu litakuwa jina lako litakuwa ibrahimu kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi
Angalia kati ya mungu na ibrahimu lilifanywa na mwenyezi mungu mwenyewe miaka mingi sana kabla ya taifa la Israeli kuwepo n ahata torati halikuwepo Zaidi sana ibrahimu alikuwa mtu wa mataifa, taifa la Israeli lilikuwa bado kubuniwa
Ahadi hizi na agano lile lilikuwa naye mwenyei mungu katika mpango wake tangu
Mbegu ya kuongezeka kwafamilia lilitimizwa katika kristo yesu mesiya
Torati nayo iliyokuja kwa mkono wa Musa aliweka muhuri agano lile kwa kuja kwake yesu ke=risto bwana wetu maana ni Yesu kristo aliyeweka sharia yote kikamilifu kuwa basi tukitubu dhambi na kuungama na kughairi mienendo yetu na kumpokea yesu mioyoni mwetu basi katika jina la utukufu na lenye nguvu la yesu sisi basihuhusishwa katika agano na ahadi ile na tuna kuwa warithi wa zile ahadi na kujitwallia uzima na uzima wa milele wokovu katika yesu kristo ndiyo nguzo ya wokovu wetu