KUTAFUTA UMOJA

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
KUTAFUTA UMOJA
Loading
/

MATUMAINI PROG 1497
TITLE: KUTAFUTA UMOJA
TEXT: WAGALATIA 2:6-10
Msikilizaji mpenzi natumai u buheri wa afya na ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha matumaini. Leo twalichambua neno kutoka waraka wa Paulo kwa wagalatia 2; 6-10 kutafuta umoja Jina langu ni david mungai, wimbo alafu tuendelee

WIMBO

Naam karibu tena twalichambua fungu la neno kutoka kwa waraka wa Paulo kwa wagalatia 2:6-10 kutafura umoja. Katika karne ya kumi na sita kanisa lilikuwa chini ya mamlaka ya serikali na sauri ya ukweli wa neno la mungu haikusikika sahihi ingawa kulikuwa na kundi ndogo lilozingatia ukweli wa neno la mungu sauti ya kanisa ilikuwa chini wakristo wakaanza kuwa na tashwishi na ni lipi hilolillilokuwa kweli, kukawa na mgawanyiko lakini umoja kwa upole na utaratibu ulitafutwa kwa udi na uvumba kuutafuta umoja ni jambo muhimu. Nasoma waraka wa Paulo kwa wagalatia 2:6-10

6 Lakini wale ambao walionekana kuwa viongozi wao, mimi sijui wala sijali kama walikuwa na vyeo gani, kwa sababu Mungu haangalii cheo cha mtu; nasema kwamba hao watu hawakuongezea cho chote katika ujumbe wangu. 7 Badala yake walitambua kwamba Mungu alikuwa amenipa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu wa mataifa mengi ne kama vile Petro naye alivyotumwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi.8 Kwa maana ilikuwa dhahiri kwamba Mungu aliyemwezesha Petro kuwa mtume kwa Wayahudi ndiye aliyekuwa akifanya kazi katika huduma yangu kama mtume kwa watu wa mataifa mengine. 9 Basi, Yakobo, Kefa na Yohana, ambao walikuwa nguzo za kanisa, walipotambua kwamba Mungu alikuwa amenijalia neema yake, walitushika mikono, mimi na Barnaba, kama ishara ya ushirikiano wetu. Walikubaliana kwamba sisi twende kwa watu wa mataifa mengine na wao waende kwa Wayahudi. 10 Walichotuomba ni kwamba katika huduma yetu tuende lee kuwasaidia maskini; jambo ambalo nimekuwa nikijitahidi kufa nya.

Kutoka kwa fungu hili la neno la mungu latuonyesha mambo kandaa ya kutazama na kuzingatia kufafanua umoja.
Jambo la kwanza, tafakai na uchunguze msimamo wa mtu Mbele zake mungu. je, ni mtu anaye zingatia mambo ya mungu namna gani, nikwa dhati au ni kwa mzaha. Uhusiano wetu na mungu ndio hutuonyesha namana ya kushirikiana na wengine na kama upeno ndio msukumi au mvuto wako utawapenda na wengine maana wewe ni balozi wake mungu. ili uipalilie umoja wako na ndugu rafta kwa maombi kuujua na kuufahamu msimamo wake katika kristo na neno la mungu
Jambo la pili, peleleza na uone namna huyo ndugu au dada anacyohudumu ni kwa sifa zake mungu. je, imjili anayoihubiri yazingatia ukweli wa neno la mungu? petro ma ishuhuda wake aliutia nguvu ushuhuda wake Paulo maana utumishi na huduma wao ni kwa bwana yesu aliye mwokozi wa wote
Jambo la tatu; tuchunguze kama kwelikama twamtumikia bwana mmija au kana kwamba twazitumikia tamaa za miili yetu
Paulo kefa yohana n ahata yakobo walimtumikia bwana mmoja aliye, yesu kristo na kwa utukufu wa mungu baba aliye mbinguni
Umoja wetu uliyo mkuu na maana twaupata katika kristo maana tu viungo vya mwili mmoja. Tumawe yaliyohai ya jingo moja kanisa la bwana wetu yesu kristo la kote duniani hebutafakari kifo chake kristo bsalabani, hebu fikiria mateso na masumbuko yake bustani mwa getsemane fikiria damu aliyomwaga msalabani alipoisalimu roho yake akalia Imekwisha
Hebu fikiri kwamba siku ya tatu mugnu baba alimfufufa yesu kutoka kwa wafu. Akaonekana na ndugu wengi baada ya kufufka kwake kabala ya kupaa kwake nbinguni
Huo ndio msigi imara wa umoja wetu

OMBI
Endapo waihitaji msaada wetu Zaidi rafadhali wasiliana nasi, anwani na nambari zet za simu ntazisoma baada ya wimbo huu
WIMBO
MATUMAINI
TWR
SLP 21514-00505
NAIROBI KENYA
SIMU: 072170520
BARUA PEPE: letters@twr.co.ke
Jina langu ni David Mungai, kwaheri kwa sasa.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!