Jinsi uovu huenea

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Jinsi uovu huenea
Loading
/
Mwanzo 6:4-7

Hujambo. Karibu katika kipindi hiki cha matumaini. Leo twalichambua neon kutoka Mwanzo 6:4-7 na tutajifunza jinsi uovu huenea. Naitwa David Mungai. Msikilizaji, nilipokuwa kijana, baba na mama walikuwa wakulima shupavu. Wakati wa kuvuna kama ni viazi au mahindi ilitupidi kuchagua tena kwa makini kuondoa viazi, hata kama moja kuondoa kama imeoza kwa sababu ingeharibu ngunia nzima. Na hivyo ndivyo ilivyo na maisha yetu mtu mmoja mwovu aweza kuwaambukiza wengi uovu wake na uovu hueneza na kusambazwa. Katika kitabu cha mwanzobtwaona vile uovu ulienezwa, n ahata waleo mbinu ndiyo hiyo. Mwanzo 6:4-7

Nao wanefuli walikuwako duniani siku zile, tena baada ya hayo wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu wkazaa nao wana hao ndio waliokuwa watu hodari zaman, watu wenye sifa. Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani akahuzunika moyo. BWANA akasema nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi: mwanadamu na mnyama na kitambaacho na ndege wa angani kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.

Hapa twapata mawazo kadhaa yanayoweza kutusaidia kuona namna uovu huenea. Kulikuwepo wanafiki, majitu ya watu. Wana wa Mungu wakaoa binti za watu, wakawazaa wato hodari wakati ule. Wana wa Mungu walikuwa uzao wa Sethi maana alikuwa mcha Mungu. Binti za watu.

Waliuwa wa ukoo wa kaini, aliyemuua ndugu yake Habili. Kwa hiyo kukawepo ndoa kati ya wasiomcha na waliomcha Mungu. Wanafili majitu watu wakaanza kuwanyanyasa walio wanyonge. Na hata waleo tunao wakubwa kimwili wakubwa katika vyeo vyao kazini, na haya tumeyaona na kuyasikiabyakizungumzwa. Na uovu huo haukumpendeza Mungu n ahata wa leo haumpendezi. Maovu ya kiakili na kimwili nayakawa hayo ndiyo maisha. Na Mungu akahuzunika… “BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwandamu duniani akahuzunika moyo.” Na Zaburi 14, twasoma ya kwamba Mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu. Wameharibu matendo yao na kuyafamya chukizo. Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu aone kama yuko mtu mwenye akili amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka wameoza wote pamoja. Hakuna atendaye mema La: hata mmja. Je, wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walayo mkate, hawamwiti BWANA. Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi; maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki. Msikilizaji tukiendelea kutenda maovu, tutaadhiriwa na ni hasara kwa maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki. Hayo ndiyo maombi yangu kwamba kw kutubu na kuungama dhambi zetu, na kuoshwa na damu ya Yesu tutakuwa kizazi cha haki. Katika familia zetu kanisani na katika shughuli zetu za ujenzi wan chi tutakuwa watu wenye haki maana Mugu ametuahidi kuwa pamoja nasi wenye haki. Kwa kumjua na kumpokea Yesu, basi tuipokee neema yake Mungu tena kwa Imani.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!