Uwe Wa Kuaminika

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Uwe Wa Kuaminika
Loading
/
Mwanzo 41:45-57

Hujambo msikilizaji. Hiki ni kipindi cha kujifunza neon la Mungu. Biblia. Leo twalipata neon letu kutoka mwanzo 41:45-57.


Tunao watu sabuli mbalimbali. Kunao watu waaminifu na kunao wengine huwezi kuwaamini. Na wewe je? Kama kweli wahisi kwamba waweza kuaminika basi umshukuru mungu na wewe ni kinyume cha hayo nakuambia wazi ya kuwa nafasi ipo ya kubadilishwa, na nguvu za mwenyezi mungu.

Nasoma somo letu kutoka mwanzo 41:45-57. Hili ni fungu la neon la mungu linalotuonyesha ya kwamba, kati ya wana wa yakobo palikuwa na mmoja aliyeaminika, jina lake Yusufu. Nasoma kutoka Mwanzo 41:45-57

Farao akamwita Yusufu Safenath panea akamwoza Asenathi binti Potifera, kuhani wa Omi, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri. Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini aliposimama mbele ya uso wa Farao akapita katika nchi yote ya Misri. Ikawa katika miaka ile saba ya shibe nchi ikazaa kwa wingi. Akakusanya chakula chote cha miaka ile. Saba katika nchi ya misri. Akaweka chakula katika miji chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake. Yusufu akakusanya nafaka kama mchangaa wa pwani nyingi mno, hata akaacha kuhesabu, maana ilikuwa hauna hesabu. Kabla ya kuja miaka ya njaa Yusufu akazaliwa wana wawili, ambao Asenathi binti Polifera, kuhani wa Oni, alimzalia.

Yusufu akamwita jina lake yule aliyezaliwa kwanza manase maana alisema Mungu amesahaulisha taabu zangu zote, na nyumba yote ya baba yangu. Na wa pili akamwita jina lke Efraimu maan alisema Mungu amenipa uzazi katika nchi ya mateso yangu. Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika nchi ya misri. Ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa kama vile Yusufu alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote bali katika nchi yote ya misri palikuwa na chakula. Na nchi yote ya misri ilipoona awape chakula. Farao akawaambia wamisir wote, enendeni kwa Yusufu atakavyowaambia fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote akawauzia wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wan chi zote wakaja misri kwa Yusufu ili wanunue nafaka kwa sababu njaa imekuwa nzito dunia yote

Hapa twaona ya kwamba; kwa sababu ya kuaminika kwake Yusufu, na kutafsiri ndoto za Farao, Farao alilibadili jina la Yusufu na kumwita Safenath-panea maana yake anayefunua mambo ya siri, watu wasije kumshuku. Pamoja na hayo kamwoza mmoja wa binti za kuhani kwake Yusufu. Kwa hiyo Yusufu akapata jina jipya na mke. Mungu akambariki Yusufu na wanawe wawili, Manase na Ephraimu. Maana yake Manase ni, mungu amenisaidia kasau taabu za familia yangu na shida zote. Mwana wa pili aliitwa Efraimu maana yake: Mungu ameniwezesha kuzaa matunda nikiwa katika nchi ya shida na dhiki.

Somo letu ni kwamba; aliyemwaminifu Mungu hupokea mem ahata katika dhiki ya kiwango cho chote. Na tukunbuke ya kwamba Yusufu aliaminika kwa sababu alikuwa mcha Mungu. Hata nasi, mungu ana uwezo kutufunikia mengi kwa sabbau ya kuwa wamiinifu. Dini na nguvu za kimwili ni kwa neema yake mungu pekee. Zaidi twajifunza ya kwamba kwa sababu ya uaminifu wake Yusufu hata nchi ilitoa mazao maradufu na neno la mungu lasema; ….Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia wamisri.

Mapendekezo yote ya Yusufu na mipango yake zikafanikisha nchi yote ya misri kuikabili njaa kwa sababu aimhuzisha mungu. Hakufanya kwa nguvu na elimu yake mwenyewe bali alimwomba mungu amuezeshe. Si kuomba tu, bali akawa mnyenyekevu.

Ukiwa mnyenyekevu na mwaminifu mbele zake mungu; mungu mwenyewe atakukweza kwa njia yake. Na hiyo ni siri na somo kuu. Kweli. Mungu atakusaidia kwa mwaminu katika mipango yako ya kifamilia kazini n ahata katika kanisa. Neno lasema “ basi nyenyekeeni chini ya mkono ulio hodari wa mungu, naye atakukweza kwa wakati unaofaa.” Mwachie mungu!! Kwa sala na maombi na shukrani.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!