Matokeo Ya Wivu – Part 2

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Matokeo Ya Wivu - Part 2
/
Mwanzo 37:28-36

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha matumaini na katika kipindi hiki sisi hulichambua neno mungu lililo hai. Leo twalichambua neno kutoka mwanzo 37:28-36 jina langu ni David Mungai.

Wivu ni mbaya sana na matokeo yake huudhi na kudhuru. La kushangaza ni kwamba tangu jadi mwanadamu ameishi na wivu na matokeo yake husababisha hasara kubwa maishani mwetu na hata kwa jirani. Kwa sababu ya wivu, kaini alimwua ndugu yake habili. Wivu ni mbaya mfalme solomoni/suleimani kwa hekima yake yote, aliandika Mithali 6:34 “Maana wivu ni ghadhabu ya mtu. Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.”

N akatika kitabu cha wimbo ulio bora 8:6. Suleimani aliandika. “nitie kama muhuri moyoni mwako, kama muhuri juu ya mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama mauti na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, na miali yake ni miali ya Yahu”


Lazima tujihadhali na wivu ni moto unaounguza, na kuchoma. Hili ni jambo la kutilia maanani sana. Nasoma kutoka Mwanzo 37:28-36

“Wakapita wafanya biashara wamidiani. Basi wakamtoa Yusufu wakampandisha kumtoa katika birika wakamwuza Yusufu kwa waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini nao wakamchukua Yusufu mpaka misri. Akarudi reubeni birikani kumbe! Yusufu hayumo katika birika, akararua nguo zake. Akarudi kwa ndugu zake akasema mtoto hayuko, nami niende wapi? Wakitwaa kanzu ya Yusufu wakachinja mwanambuzi na kuichovywa kanzu katika damu. Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao wakasema, tumeona hii basi utambue kama kanzu hii ni ya mwanao ama siyo. Akaitambua, akasema ndiyo kanzu ya mwanangu mnyama mkali amemla bila shaka Yusufu ameraruliwa. Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni na kumlilia mwanawe siku nyingi. Wanawe wote na binti zake wote wakaondoka wamtulize lakini akakataa kutulizwa akasema, La! Nitamshukia mwanangu nikisikitika hata kuzimu. Baba yake akamlilia. Nao wamidiani wakamwuliza huko misri kwa potifa akida wa Farao, mkuu wa askari”

Hiyo basi ndio habari ya wana wa Yakobo waliomwuza ndugu yao yusufu kwa waishmaeli waliokuwa safarini mwao. Hapa basi twapata matokeo kadhaa.

Taabu na shida: tumesoma ya kwamba reubeni aliporudi mle shimoni kumtoa ndugu yake yusufu alikuta tayari alikuwa ametolewa na ndugu wengine na kuuzwa kama mtumwa kwa waishmaeli. Reubeni alikuwa na mpango wa kumtoa Yusufu shimoni na kumrudisha kwa baba yao. Yakobo. Reubeni alikasirishwa sana, kwa ndugu yake, kuuswa kwa vipande ishirini vya fedha. Mambo hayo yalimkasirisha sana reubeni. Akaghadhabika sana moyoni hata akasema. “mtoto hayuko, nami niende wapi?” kumwuza yusufu hakukuleta suluhisho maana ndugu wengine. Bado walioweka wivu mioyoni mwao.

DHIHAKA: wivu mioyoni mwa wale wana wa Yakobo ulisababisha dhihaka. Walimchinja mbuzi wakaiweka ile kanzu ya yusufu madoadoa ya damu. Ionekane kana kwamba mnyama alimua yusufu. Wakapangapanga vile watamdanganya baba yao. “Tumeona hii, basi utambue kama kanzu hii ni ya mwanao ama siyo.” Lakini reubeni hakupendezwa n ajambo hili. maombolezi. Walipomletea baba yao ile kanzu. Yakobo aliitambua kwamba ni ile ya mwanawe Yusufu, hata akasema. “Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla bila shaka Yusufu ameraruliwa.” Huo ukawa mwanzo wa maombolezi ya yakobo. Akaomboleza kwa miaka mingi. Kwa sababu ya wivu, wana wa yakobo wakamletea huzuni na kusononeka kwa miaka mingi. Wivu ni mbaya sana, ndugu au dada msikilizaji.