Tufanye Nini Tunapokubwa Na Makosa

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Tufanye Nini Tunapokubwa Na Makosa
/
Mwanzo 39:7-23

Hujambo. Ni wakati wa kujifunza neno la mungu. Mwanzo 39:7-23. Tufanye nini tunapokubwa na makossa? Jina langu ni David mungai. Biblia ni kitabu cha kipekee maana ni neno la Mungu na ni katika kitabu hiki mungu ametuambia matarajio yake kutoka kwetu. Katika biblia twapata yanayompendeza. Kwa mfano, |Amri kumi za mungu. Usimwabudu mungu mwingine awaye yote.

Kwa miaka kadhaa watu wamekuwa wakisema hamna shida kupeana talaka hamna shida katika ngono kati ya mwanaume na mwanamume, mwingine hata Wanyama hawafanyi hivyo. Ni makossa na ni dhmabi. Dhamiri zetu huonyesha yatiyo mema maovu na mabaya. Ujumbe wetu wa leo waonyesha namna ya kufanya tunapokubwa na makossa au mambo mabaya. Katika kitabu cha mithali 1:10 twapata maneno haya “ Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi wewe usikubali. Na mithali 4:14-15 “Usiingie katika njia ya waovu. Wala usitembee katika njia ya wabaya. Jiepushe nayo, usipite karibu nayo. Igeukie mbali ukaende zako.”


Hata hivyo kunao wachache ambao tabia na desturi zao sio mbaya vile, na huburudisha kama hewa safi. Yusufu alikuwa hivyo kwa baba yake, na alipouzwa kwa potifa kama mtumwa, akawa kama harufu nzuri nyumbani kwa potifa. Kazi yake na umbo lake. Yote mawili yalimpendeza mwajiri wake, hata mke wa potifa akamtamani kwa sabau neema ya mungu ilikuwa juu yake. Hata mke wa potifa akatamani kulala na Yusufu. Nasoma kutoka Mwanzo 39:7-23


“Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, lala nami. Lakini akakataa akamwambia mke wa Bwana wake, tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanye ubaya huu mkubwa nikamkose mungu? Akawa akizidi kusema na yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa siku moja akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani, huyo mwanamke akamshika nguo zake akisema, lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia nje. Ikawa alipoona ya kwamba amemwachilia nguo yake mkononi mwake, naye amekimbia akawaita watu wa nyumbani mwake aksema nao akinena, angalieni ametuletea mtu mwebrania atufanyie dhihaka. Ameingia kwangu ili alale nami nikalia kwa sauti kuu. Ikawa aliposikia ya kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliacha nguo yake kwangu, akakimbia, akatoka nje. Nasi akaiweka ile nguo kwake hata bwana wake aje nyumbani. Naye akamwambia kama maneno hayo akisema yule mtumwa mwebrania uliyemleta kwetu aliingia kwangu anidhihaki. Ikawa nilipopaza sauti yangu, nikalia, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje. Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliymwambia akisema, mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka.

Bwana wake akamtwaa yusufu akamtia gerezani mahali walipofungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani. Lakini BWANA akawa pamoja na yusufu akamfadhili akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza. Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa yusufu watu wote waliofungwa waliomo gerezani na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya. Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mokoni mwa yusufu. Kwa kuwa BWANA alikuwa pamoja naye. Bwana akayafanikisha yote aliyofanya.

Ni jambo la kupendeza na la kutia moyo, kumwona mmoja aliyesimama wima katika majaribu. Yusufu alijua siri na akawa shujaa kuitekeleza. Alikataa kata kata kuangukia dhambi ya uzinifu. Ndiyo hatukatai kwamba yusufu alikuwa mzuri, aliyetamanika lakini alikataa kujiingiza ndani ya dhambi ya uasherati. Dhambi ya uasherati hutendeka kwa dakika chache lakini baada ya hayo, huacha. Vilema na makovu moyoni na akili na Zaidi hukatiza maendeleo ya mtu maishani. Ni wengi wamefupisha Maisha yao kwa sababu ya uasherati uzinifu. Uasherati husababisha hata vifo vya mapema mno. Afadhali kuwekwa jela kama yusufu na ukweli wa mambo udhihirike. Jambo la pili. Tumeona ya kwamba; yusufu aliposhikwa na yule mama, yusufu alikimbia akamwachia mama koti mkononi. Unapojaribiwa katika dhambi jaribu sana kuukimbia ile dhambi. Acha kulegalega hapo. Kimbia toka mahali hapa mahali pa dhambi. Jambo la tatu- baada ya kuikimbia dhambi. Yusufu aliendelea kuwa mwmainifu katika na kuwatendea wengine haki na kwa uaminifu wake. Potifa alimpa mamlaka Zaidi katika nchi ya misri.

Heri kuishi Maisha ya adilifu na kwa uaminifu, na mungu atakukweza kwa wakati wake. Mother Teresa alisema, Maisha yako ndiyo ujumbe unaosomwa na wenzako. Nakuombea uwe shujaa katika kukataa kutenda dhambi.