Dhambi Ni Ugonjwa

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Dhambi Ni Ugonjwa
/
Warumi 3:9-20

Hujambo na karibu

Leo twalitambua mungu ila neno la mungu kutoka waraka wa paulo kwa Warumi 3:9-20. Dhambi ni ugonjwa

Jina langu ni David Mungai, Karibu wimbo alafu tuendelee.

Wimbo

Naam, Karibu tena

Magonjwa ni mengi duniani kwa mfano,kipindupindu,saratani,malaria na kadhalika.

Lakini kunao ugonjwa mbaya zaidi ,nao ni ugonjwa wa moyo ugonjwa wa dhambi ipo duniani kote.

Nasoma neon kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 3:9-20

9 Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine?La ! hata kidogo kwa maana tumekwisha kuwashitaki wayahudi na wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi.

10 Kama ilivyoandikwa kuwa ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.

11 Hakuna afahamiye,Hakuna amtaftae mungu.

12 Wote wamepotoka wameoza wote pia, Hakuna mtenda mema La! Hata mmoja.

13 Koo lao ni kaburi wazi kwa ndimi zao wametumia hila sumu ya rira chini ya midomo yao

14 Vinya vyao vimejaa laana na uchungu.

15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu.

16 Uharibu na mashaka yamo njiani mwao.

17 Wala njia ya amani hawakuijua.

18 Kumcha mungu hakupo machoni pao.

19 Basi twajua yakua mambo yote inenayo torati huyanena kwa wao walio chini ya torati ila kila kinywa kihumbwe na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya mungu.

20 Kwasababu hakuna mwenye mwili atakaehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

Dhambi ni ugonjwa kwa kila mtu duniani ni mgonjwa wa dhambi.Nasoma tena maneno ya mstari wa 9.

Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La ! Hata kidogo kwa maana tumekwisha kuwashitaki wayahudi na wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi.

10 Hakuna mwenye haki hata mmoja wote tu wagonjwa wa dhambi.

Jambo la pili ni kwamba dhambi ni kwa kila mmoja wetu na mshahara wa dhambi ni mauti na dhambi zetu zilisababisha kifo cha yesu cha msalabani- mtu mwenyewe binafsi akitubu husamehewa na kuhesabiwa haki.

Nasoma maneno ya mstari wa 13 na 14

Koo Lao ni kaburi wazi

Kwa ndimi zao wametumia hila, sumu ya tira i chini ya midomo yao,

Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu kila mmoja wetu binafsi ni mwenye dhambi.

Jambo la tatu ni kwamba dhambi ni kila mahali duniani kote na hivyo ndivyo ilivyo maneno ya mstari wa 19-20

Basi twajua ya kwawa mambo yote inenavyo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati.

Ila kila kinywa ihumbwe na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya mungu.

Kwasababu hakuna mwenye mwili atakaehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

Neno la mungu ni kweli na ukweli wa neno la mungu na ukweli huo ni wa kudumu-Dhambi hairudishwi nyuma lakini huondolewa na kwa damu ya yesu kristo alipoangikwa msalabani.