Jinsi Ya Kutosheleza Sheria Ya Mungu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Jinsi Ya Kutosheleza Sheria Ya Mungu
Loading
/
Warumi 8:1-4

Hujambo na karibu tujifunze neno la mungu kutoka kitabu cha warumi 8:1-4 jinsi ya kutosheleza sheria ya mungu. Jina langu ni david mungai. Karibu wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena tujifunze neno pamoja. Waraka wa Paulo kwa waroma 8:1-4, swali tunalojiuliza kila mara ni hili, mtu awezaje kuweka au kutii sheria yote? Nasoma waraka wa Paulo kwa Warumi 8:1-4

1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;

4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;

4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

Kutoka kwa fungu hili la biblia, mtume Paulo atufundisha na kutuonyesha matendo tunayopaswa kufanya ili kutosheleza sheria ya mungu

Lazima tuenende katika roho mtakatifu. Sheria takatifu za mungu zatuhukumu maana kila moja wetu ni mwenye dhambi. Tumekosa wala hatuna uwezo wa kutii sheria na matendo yetu twahukumiwa na sheria kwa sababu tu wanyonge na hafifu lakini kwa Imani katika yesu kristo tumeondolewa hukumu mstari wa kwanza

1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

Kristo aliyakamilisha matakwa yote ya sheria na kwa kumwamini yesu tumehesabiwa haki na mstari wa pili watuonyesha ya kwamba twapaswa kuenenda katika roho mtakatifu naye roho mtakatifu kutuelekeza katika neno lake mungu. Maana neno la mungu wetu kimaisha na ndiyo mwanga wa njia zetu.

Jambo la pili lazima tusherehekee njia ya krist. Sheria ya dhambi hufanya kazi na mwili lakini roho wa mungu hufanya kazi na neno la mungu ndio upanga ukataokuwili kati Maisha yetu

Yesu mwenyewe alilikariri neno kumshinda shetani. Imeandikwa akamshinda shetani, tusherehekee ushindi wa bwana wetu yesu kwa sababu baada ya kuangikwa msalabani alizikwa siku ya tatu akafufuka. Twasherehekea ushindi wa ufufuo maana ndiyo ilivyo hata sisi baada ya kufufliwa kutoka kwa wafu alikaa hapa duniani siku harubaini akiwaonyesha wanafunzi wake keli alifufuka kimwili hatimaye akapaa mbinguni na huko ndiko atawaandalia arudipo kutuchukua nasi tuwepo. Ni sherehe kweli ingawa kristo aliteswa

Jambo la tatu lazima tujitwalie kwa Imani kazi yake mungu

3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;

Na katika kristo yesu Maishani mwetu tumehesabiwa haki. Tumekuwa maskani yake roho matakatifu wa mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!