Upendo Wa Mungu Kwa Wasiopendeka

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Upendo Wa Mungu Kwa Wasiopendeka
/
Warumi 5:6-11

Hujambo msikilizaji wangu popote ulipo. Jina langu ni david mungai. Nakukaribisha tujifunze neno pamoja warumi 5:6-11, upendo wa mungu kwa wasiopendeka. Karibu wimbo halafu tuendelee kujifunza pamoja.

Wimbo

Naam karibu tena twalichambua neno kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 5:6-11 upendo wa mungu kwa wasiopendeka

Upendo upo duniani kote na upendo upo ndani ya watu, upendo ni aina mbalimbali

  1. Kuna upendo wa kimwili au upendo wa nyama
  2. Kuna upendo wa kifamilia upendao kwa mama, kwa watoto, baba na mama
  3. Kuna upeno wa mwanaume kwa mwanamke
  4. Na kuna upendo unaotoka kwa mungu unaowapenda watu wote hata wale wasiopendeka

Na huo ndio upendotuliopata hapa katika fungu hili la neno la mungu warumi 5:6-11 nasoma

6 Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.

7 Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.

8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.

10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.

11 Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.

Ili tuelewe upendo wa mungu Paulo aeleza jinsi tulivyokuwa alipotupenda mungu

Jambo la kwanza hatukumjua mungu a hata katika waraka huu kwa wrumi 3:23, twasoma kwamba sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa mungu

Ni rahisi mtu kujitoa kufa kwa ajili ya mtu mwema lakini kujitoa kwaajili ya mtu mbaya na mwovu ni vigumu. Lakini licha ya kuwa sisi tulikuwa na dhambi bado tu yesu kristo kwa sababu ya kutupenda alijitoa kufa msalabani kwa ajili yetu ili tukimwamini tupate ondoleo la dhambi.

Neno limesema kwamba warumi 5:8

Bali mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi kwa kuwa kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi tulikuwa wenye dhambi.

Maneno ya mstari wa 9 yatuonyesha vile upendo huo wa mungu hufanya kazi

9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.

Mwenye dhambi, wewe na mimi msikilizaji huhesabiwa haki Mbele ya macho ya mungu tunapooshwa na damu ya yesu pamoja na hayo katika mstari wa kumi, twaona yakwamba mugnu alitupenda sana tulipokuwa maadui wake mungu

10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake

Kwa kumpokea yesu na kumkiri kwa midomo yetu mungu ametupokea kuwa marafiki na hiyo ndiyo furaha na raha yetu upokee kwa Imani upendo huu wa mungu siyo kufani.