Mungu Ni Kweli

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Ni Kweli
Loading
/
Warumi 3:1-8

Hujambo msikilizaji. Karibu tujifunze neno la Mungu pamoja. Twalichambua fungu la neno la Mungu kutoka Warumi 3:1-8

“Mungu ni kweli”kabla ya kuendelea mbele tufurahie wimbo.

Naam karibu tena twalichambua neno kutoka kwa fungu la neno kutoka waraka wa Paulo kwa warumi 3:1-8. “Mungu ni kweli”

Hakuna mtu ampendaye mtu mwongo,maana huwezi kumwamini. Lakini daima Mungu, daima ni kweli na ahadi zake ni kweli

Nasoma kutoka waraka Warumi 3:1-8

1 “basi myahudi ana ziada gani? Wa kutahiriwa kwa faa nini?”

2 kwa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia(oracles)ya Mungu.

3 ni nini,basi,ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutawabadili waaminifu wa Mungu? La hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo,kama ilivyoandikwa, ili ujulikanekuwa una haki katika katika maneno yako ukashinde uingiapo katika hukumu.

4 lakini ikiwa udhalimu wetu waidhibitisha haki ya Mungu;tuseme nini?je,Mungu ni dhalimualetaye ghadhabu?(nasema kwa jinsi ya kibinadamu)

5 hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuhukumu ulimwengu?

6 lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu wa uongo wangu,mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?

7 kwa nini tuseme (kama tulivyosingiziwa,na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo) na tufanye mabaya ili yaje mema?ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.

8 katika fungu hili la neno la Mungu, Paulo alionyesha vile Mungu alivyo wa kweli.

(1) Kwa kutupatia Torati faida yake torati ni nini? Jibu twapata. Mstari wa pili “kwafaa sana kwa kila njia kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia za Mungu”

Na je kutokuamini kwetu kutaubadili uaminifu wa Mungu kwetu? Jibu lapatikana katika mstari wa 4.

“la hasha!” Mungu ni daima mwaminifu na si mwongo.

Jambo la pili kwamba kwa vile Mungu huhukumu dunia haki ya utakatifu wake huonekana. Na Ataihukumu dhambi,maana amesema,”mshahara wa dhambi ni mauti”

Kama ulivyo kweli na hukumu yake ni kweli.

Hata kwa mwenye dhambi atatoa hukumuya kweli Msf 4

“lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?

Hata wengine hudhani ya kwamba Mungu hawezi mhukumu mwenye dhambi eti kwa sababu

Mungu ni upendo, Mungu ni upendo, ndiyo, lakini dhambi ni chukizo kwake kwa hivyo, mwenye dhambi asipotubu dhambi lazima atahukumiwa.

Dhambi ni chukizo kwake Mungu. Mungu ni kweli na kweli,ataihukumu dhambi maana hasemi uongo. Njia ya pekee ya kuondoa hukumu hii ni kutubu na kuungama dhambi na kughairi mienendo yetu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!