Ibrahimu Nyayo Zake Za Imani

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Ibrahimu Nyayo Zake Za Imani
/
Warumi 4:6-12

Hujambo na karibu. Jina langu ni David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha matumaini. Leo katika kipindi twalichambua fungu la neno kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 4:6-12. ‘IBRAHIMU- NYAYO ZAKE ZA IMANI’

Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena. Ibrahimu alikuwa na hata wa leo ni baba wa Imani kwa watu wengi. Swali ni hili: Twawezaje kufuata nyayo zake?

Wengi twajua, Mungu yupo, lakini swali ni ‘Nilikujua au ni kuamini, au ni yote mawili?’ Tufuate nyayo zake Ibrahimu namna gani? Mtume Paulo aliwaandikia wakristo wa kirumi, aliwakumbusha na kuwapa mfano mwema wa kuiga- mfano wa Ibrahimu. Nasoma waraka wa Paulo, kwa Warumi, 4:6-12.

Warumi 4:6-12

Naye Daudi asema hivi juu ya furaha ya mtu yule ambaye Mungu amemkubali kuwa mwadilifu bila kuyajali matendo yake:

7 “Heri wale waliosamehewa makosa yao ambao makosa yao yamefutwa.

8 Heri mtu yule ambaye Bwana hataziweka dhambi zake katika kumbukumbu.”

9 Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”

10 Je, Abrahamu alikubaliwa kabla ya kutahiriwa, ama baada ya kutahiriwa? Kabla ya kutahiriwa, na si baada ya kutahiriwa.

11 Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini Mungu, wakafanywa waadilifu.

12 Vilevile yeye ni baba wa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwa wametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njia ileile ya imani baba yetu Abrahamu aliyofuata kabla ya kutahiriwa.

HATUA ZAKE IBRAHIMU ZA IMANI

(1) Kila mmoja wetu, tuna haja ya kuenenda kwa Imani. Yeyote awaye na haja ya Imani, hutafuta msamaha wa dhambi , kama anavyosema Daudi katika Zaburi wa 32:1 “Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake.” Hatua ya kwanza ya kuzingatia Imani ni kutubu na kuungama dhambi zetu. Mungu huichukua dhambi na kwa hivyo lazima tutafute kusamehewa dhambi.

(2) Hatua ya pili: Tuna change moto kutembea kwa Imani kama tunavyosoma katika mstari wa Warumi 4:9 Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Kwa ufupi ni kusema. Si kwa nguvu za mtu kibinafsi zinazofaulu kuleta Imani bali ni kuwa na kiu cha kumjua na kumkiri Yesu kwa Imani moyoni na kumruhusu Bwana atawale maisha yako. Hiyo ni hatua ya pili nay a muhimu sana , maana twaenenda kwa Imani. Hatari ipo kuwa ukitubu dhambi shetani kumnyemelea mtu na kumkumbusha dhambi za zamani na kumwonyesha mtu kuwa ni ngumu kusamehewa. Nayo si kweli, kwa sababu akisha kusamehewa dhambi na Mungu hazi, Mungu kamwe hatazikumbuka. Chukua hatua ya Imani na uishi kwa Imani na hutasikiliza sauti ya mwovu shetani. Hatua ya tatu. Kuna mwelekeo katika safari ya Imani kama ilivyosoma. Mst 11. Warumi 4:11

“Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini Mungu, wakafanywa waadilifu.”

Kwa kuungama kutubu na kumwamini ‘Mungu Ibrahimu aliyehesabiwa haki kabla ya kutahiriwa. Kutahiria kulikuwa ni kuweka muhuri , ikawa ni agano kati ya Ibrahimu na Mungu.

Mungu akiwa na agano na mtu hilo agano la milele kama vile mtu hawezi kuondoa tohara. Na hii ndiyo mstari wa 12, wasema hivi. ‘tena awe baba ya kutahiriwa kwa wale ambao si waliotahiriwa tu bali pia wanazifuata nyayo za Imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa.

Kuzifuata nyayo za Ibrahimu ni vema lakini kwa nguvu zetu hatuwezi lakini kwa nguvu zetu hatuwezi lakini kwa kumwamini Mungu anao uwezo wa kutuelekeza. Mungu ameyakamilisha yote kwa kifo chake Yesu, ametutengenezea njia ya Imani kwa kumwamini Yesu. Tukisimama katika ahadi zake Mung utu washindi.