Ukijua Wajibika

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Ukijua Wajibika
Loading
/
Warumi 2:17-29

Hujambo na karibu. Jina langu ni David Mungai na leo twalitazama neon pamoja kwa redioWaraka wa Paulo kwa Warumi 2:17-29 “UKIJUA WAJIBIKA” Karibu wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, natumai umeburudishwa na wimbo huo “Ukijua wajibika kutenda” Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa uwezo au mamlaka ya kuwajibika vilivyo. Pamoja na hayo tumepewa mamlaka ya kuchagua namna ya kutekeleza wajibu wetu. Ukishayajua mambo, sharti tuwajibike vilivyo. Na tusipowajibika ni sisi wa kulaumiwa. Nasoma neno kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 2:17-29

Na wewe, je? Wewe mwenyewe unajiita Myahudi; unaitumainia sheria na kujivunia kuwa wa Mungu;

18 kwa njia ya sheria unajua matakwa ya Mungu na unaweza kuchagua jambo jema;

19 wewe unajiona kuwa kiongozi wa vipofu na mwanga kwa wale walio gizani;

20 unajiona kuwa mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa wale wasiokomaa bado. Unayo katika sheria picha kamili ya elimu na ukweli.

21 Basi, wewe unawafundisha wengine; kwa nini hujifundishi wewe mwenyewe? Unawahubiria wengine wasiibe, lakini kumbe wewe mwenyewe unaiba.

22 Unasema: “Msizini,” na huku wewe unazini; unachukia sanamu za miungu hali wewe unajitajirisha kwa kuiba katika nyumba za miungu.

23 Kwa kujigamba ati unayo sheria ya Mungu, je huoni kwamba kwa kuivunja sheria unamdharau Mungu?

24 Kama vile Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Watu wa mataifa mengine wamelikufuru jina la Mungu kwa sababu yenu nyinyi Wayahudi!”

25 Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kama ukiitii sheria. Lakini kama unaivunja sheria, basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa.

26 Kama mtu wa mataifa mengine ambaye hakutahiriwa akitimiza matakwa ya sheria, hakika atafikiriwa kana kwamba ametahiriwa.

27 Watu wa mataifa mengine watakuhukumu wewe Myahudi kama ukiivunja sheria, ingawaje unayo maandishi ya sheria na umetahiriwa, hali wao wanaitii sheria ingawahawakutahiriwa.

28 Ndiyo kusema, si kila anayeonekana kwa nje kuwa Myahudi ni Myahudi wa kweli, wala mtu hawi Myahudi wa kweli ati kwa kuwa ametahiriwa kimwili.

29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishi ya sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu.

Basi neon ndilo hilo- kumbuka ya kwamba mada yetu ya leo ni “Ukishajua wajibika”. Wayahudi wapewa torati na neon limesema kwamba walijivunia hiyo torati. Tumepewa neon la Mungu na wito mkuu kulitilia hilo neon maanani na kuwajibika la sivyo halitatufaidi. Tunayo faida kubwa kulitafakari na kulitilia maanani neno.

Daudi wa zamani alisema “ Neno lako ni taa ya miguu yangu; na ni mwanga wa njia yangu.” Na kuanzia mstari huu wa zaburi ya 119 yaani mstari 105-112, mwandishi wa wimbo huu aapa kuzingatia mawaidha ya neno la Mungu. Ukishajua, wajibika kutekeleza, maana neno ndilo kweli.

Jambo la pili ni kwamba mtu anapojua na kuarifiwa hupata sababu ya kugeuzwa. Anapofahamishwa, ‘mshahara wa dhambi ni mauti basi ni muhimu kutafuta njia na mbinu za kuepuka, kuondoa ghadhabu ya dhambi.

Mst 24. “Kama vile Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Watu wa mataifa mengine wamelikufuru jina la Mungu kwa sababu yenu nyinyi Wayahudi!” Kwa kifupi ni kusema kwamba ni vizuri kushuhudia ya kwamba Yesu ni Mwokozi kwa mdomo na kwa vitendo , la sivyo tutawakwaza wengi.

Pamoja na hayo, tufanye upya nia zetu. Neno la Mungu ndilo pekee lenye nguvu za kubadilisha nia zetu na kuzifanya upya. Na sikulijua neno peke yake bali ni muhimu kulitii ili ufanye mapenzi ya Mungu tupate kuhesabiwa haki. Tusijigambe na mambo kama tohara ya mwili, tohara ya kiroho, ambayo maana yake ni kutenganishwa na mambo ya kimwili ya dunia, nay a yule mwovu shetani.

Jitwalie ahadi zake Mungu katika nia na matendo na utafurahia kuwa kiumbe kipya.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!