Upendo Wa Kristo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Upendo Wa Kristo
Loading
/
II Wakorintho 5:14-21

Hujambo na karibu tujifunze neno pamoja. Leo twalichambua neno kutoka 2 WAKORINTHO 5:14-21, UPENDO WA KRISTO.

Jina langu ni David Mungai.

Wimbo halafu tuendelee.

Naam, karibu tena. Twalichambua neno kutoka 2 WAKORINTHO 5:14-21, UPENDO WA KRISTO.

Nasoma sasa

14 Maana upendo wa kristo watubidisha, maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote basi walikufa wote

15 Tena alikufa kwa ajili ya wote ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi ya nafsi zao wenyewe bali kwa ajili yake yeye aliyekufa, akafufuka kwa ajili yao

16 hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili

17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama. Yamekuwa mapya

18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo naye alitupa huduma ya upatanisho yaani Mungu alikuwa

19 ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makossa yao, naye ametia ndani yetu neno la upatanisho

20 basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu

21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye

Kutoka kwa fungu hili la neno twaona ya kwamba, katika mst wa 14. Upendo wa Kristo hutubidisha

Upendo wa Kristo na upendo wa Kristo ndani yetu hutubidisha na kutuendesha ndio nguvvu zetu kwa sababu Kristo anipenda nami nampenda kwa kuwapenda watu wengine na kuwatendea mema, kwa utukufu wake yesu

Paulo akiwaandikia wakristo wa shirika au kanisa la Rumi aliweka ukweli huu, nguvu kwa maneno haya warumi 6:8

Lakini tukiwa tulikufa pamoja na kristo twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye

Basi na tumpishe Kristo atawale Maisha yetu maana hakuna hasara

15 tena alikufa kwa ajili ya wote ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake aliyekufa akafufuka kwa ajili yao

Kifo cha Kristo kilikuwa mojawapo ya mpango na kusudi ya kila mfuasi wa kristo kujifunza kujinyima na kujikana hata haki zetu kwa ajili ya wenzetu.

Yesu aliyaacha yote ya mbinguni akashuka duniani hii, kufa msalabani kwa niaba na kwa ajili yetu. Tuko mbali sana kulielewa wazo na ukweli huu maana wakristo hatupendani twaishi kwa neema yake Mungu.

Tumpata mwenzetu hawezi twapita njia za mikato tukitafuta visababu. Naomba sana tumwombe Mungu atupe mzigo wa kuwapenda ndugu zetu na tujitoe kupendana kwa nini twawategemea msaada ya nchi za ulaya hali matajiri tunao hapa hapa.

Siyo matendo makuu makuu pekee huonyesha upendo. Bali na madogo kwa upendo

Siku moja nilisafiri kwenda ujerumani kuwaona wandani kuwaona wandani wetu katika huduma hii.

Nilisafiri kwa ndege usiku nikafuka uwanja wa ndege asubuhi mchovu kweli sikujua gazeti la ule mji lilikuwa limetoa habari kwamba twafika asubuhi mama mkristo mzee alikuwa atungojea pale uwanjani na bakuli la barafu ya strawberry tukala tukaona nafuu mwili. Lile tunda likatuongeza nguvu mwili, tukaendelea mbele na safari tukaenda mji mwingine kuhubiri injili kitendo kidogo cha upendo ni cha busara kuu kati yetu

Kristo alifunza kijitoa kwa ajili ya wenzetu sio wale wazuri kwetu bali kwa wote hata maadui zetu acha wamwone kristo ndani ya matendo yako.

Kwa sababu gani?

Kwa sababu Kristo ni upendo nay u ndani yetu.

Kwa sababu kristo ametuumba upya mst. 17

Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama. Yamekuwa mapya.

19 mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makossa yao, naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

20 yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya mungu katika yeye

Kweli upendo wake yesu kristo kwetu hauna kifani na kama wafuasi wake twapaswa kuoendana hivyo.

Waombee na uwapendee wote. Maana mungu nip endo. Basi tupendane na upendo wa kristo.

Upendo ndiyo moyo wa injili. Yesu hakutenda wala kuwaza dhambi lakini alisaulubiwa kwa ajili ya wenye dhambi na tukitubu sisi husamehewa dhambi. Na hii ndiyo haki ya Mungu.

Endapo wahitaji msaada Zaidi, tafah=dghali wasiliana nasi. Anwani taisoma baada ya wimbo.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!