Tabia Katika Huduma

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Tabia Katika Huduma
Loading
/
II Wakorintho 6:1-10

Hujambo na karibu tujifunze neno pamoja. Leo twalichambua neno kutoka 2


Jina langu ni David Mungai.

Wimbo halafu tuendelee.

Naam, karibu tena. Kusema kweli, yatupasa kupalilia tabia zetu maishani mwetu na katika huduma tumekabidhiwa na mwenyezi Mungu mikononi mwetu. Na Paulo atuonyesha namna katika 2 WAKORINTHO 6:1-10, tusome neno hili,

1 Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasii msiipokee neema ya Mungu bure

2 Kwa maana asema wakati ulikubalika nalikusikia siku ya wokovu nalisikia tyazama wakati uliokubalika ndio sasa

3 Tusiwe kwazo la namna yoyote katika jambo lolote ili utumishi wetu usilaumiwe

4 Bali katika kika neno tujipatie sifa njema kama watumishi wa Mungu katika saburi nyingi katika dhiki katika misiba katika shida

5 Katika mapigo katika vifungo katika fitina katika taabu katika kukesha katika kufunga

6 Katika kuwa safi katika elimu katika uvumilivu katika utu wema, katika roho mtakatifu katika upendo usio unafiki

7 Katika neno la kweli katika nguvu ya mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kushoto

8 Kwa utukufu wa aibu na kwa kunenwa vema. Kama wadanganyao bali tu watu wa kweli.

9 Kama wasiojulikana bali wajulikanao sana kama wanaokufa kumbe tu hai kama wanaorudiwa bali wasiouwawa

10 Kama wenye huzuni bali siku zote tu wenye furaha kama maskini bali tukitajairisha wengi kama wasio na kitu bali tu wenye vitu vyote

Katika maneno ya mstari wa kwanza na wa pili Paulo atuhimiza kumpokea mwokozi Yesu Kristo sasa.

Wakati wa kumtumikia Mungu ndio sasa. Arudipo Kristo hatutakuwa na nafasi nyingine ya kuwaleta wengine kwa Kristo

Lakini Yesu atakapotupeleka kwake mbinguni hatutakuwa na lengine la kumsifu pamoja na malaika.

Kuanzia mstari wa 3-10 twaonyeshwa namna ya kuendeleza huduma ya kuhubiri injili, kwa kunmshuhudia yesu kumkiri kwa midomo na kwa vitendo vyetu.

Tusihubiri asali na vitendo vyetu ni kinyume. Tusihubiri upendo na kwa vitendo ni kuwakashifu ndugu tuwe tayari kupewa majina yasiyo yetu. Kwa mfano Paulo hakuwa mdangantifu katika mstari wa nane, walimwita Paulo mwongo , nasoma maneno hayo,

8 Kwa utukufu wa aibu na kwa kunenwa vema. Kama wadanganyao bali tu watu wa kweli.- Paulo alisimama wima kupiga vita vya injili, hakurudi myuma

Katika maneno ya mstari wa 9 twaona ya kwamba waliompinga Paulo, hawakumtambua. Liwe liwalo injili iliendelea kuenea.

Acha wakuseme wewe, zingatia ya injili iende mbele. Nilionza matatu moja imeandikwa mlangoni, wacha waseme kazi inaendelea kama mbwa wabweka

Wacha wakuseme , endelea kuhubiri injili ya bwana yesu kristo. Watasema watachoka. Watuambue wasitutambue injili ya endelea. Ndiyo sababu Pulo amalizia fungu hili la neno kwa maneno haya. Kama wenye huzuni bali siku zote tu wenye furaha kama maskini bali, tukitajirisha wengi kama wasio na kitu bali tu wenye vitu vyote

Jipe moyo hubiri injili mungu u pamoja nasi.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!