Utangulizi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Utangulizi
Loading
/
II Wakorintho 1:1-11

Hujambo na karibu. Leo twaanza mfululizo wa masomo kutoka II Wakorintho 1:1-11, “UTANGULIZI”. Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena. Leo twalitazama fungu hili la Neno. II Wakorintho 1:1-11.

Baada ya kuandika Waraka wa kwanza kwa Wakorinntho, Paulo aliona muhimu kuwatembelea washiriki wa Kanisa la Korintho kwa sababu matatizo kanisani yalikuwa bado yapo. Pamoja na hayo, Paulo akaandika waraka mwingine wa pili lakini ukapotea kama anavyosema katika sura ya 2:4

“Maana katika dhiki nyingi na taabu ya moyo niliwaandikia na machozi mengi. Si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu mlio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.”

Sasa nasoma sura ya 1:1-11

1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu kwa kanisa la Mungu, lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko katika nchi yote ya Akaya

2 Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

3 Na ahimidiwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;

4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.

5 Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu; vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.

6 Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.

7 Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.

8 Maana ndugu, hatupendi msije habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.

9 Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu,

10 aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile, tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa,

11 ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba ili kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu.

Kutoka kwa fungu hili la Neno la Mungu twapata kweli nyingi sana kuhusu Mungu wetu wa mbinguni.

Mst. 2 Baba Mungu wetu, ndiye Mungu aishiye milele. Nasoma: Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

Ukweli huo wawekwa nguvu na maneno yanayopatikana katika sura ya 3:3.

1 mnadhihirishiwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa

Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.

Tunamwamini Mungu aliye hai katika Kristo.

2 Mungu Baba yetu amejawa na neema, amani rehema na faraja.

Mst2-3

2 Neema na iwe kwenu na amani…na ahimidiwe Mungu Baba, wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema Mungu wa faraja yote.

3 Mungu Baba yetu ni mwaminifu. Mst 18. “Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si ndiyo na siyo?

4 Uwezo wake Mungu wapatikana kwa watu wake.

5 Mungu Baba ndiye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, na ndiye mwana wa Mungu. Mstari wa 19

“Maana mwana wa Mungu Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yaani, mimi na Silwano na Timotheo hawakuwa, na ndiyo na siyo bali katika yeye ni ndiyo.

Katika Kristo twamwamini Mungu aliye yeye ndiye. Mungu muumba wa mbingu nan chi na ndiye mpaji wa uzima wa milele tulio nao katika Bwana Yesu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!