Umuhimu Wa Imani

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Umuhimu Wa Imani
/
Wagalatia 3:26-29

Hujambo mpenzi msikilizaji na karibu tujifunze neno pamoja. Leo twalichambua fungu la neno kutoka waraka wa Paulo kwa Wagalatia 3:26-29, UMUHIMU WA IMANI jina langu ni David Mungai kabla hatujaendelea Zaidi furahia wimbo huu tuendell

Naam karibu tena tujifunze neno waraka wa Paulo kwa Wagalatia 3:26-29 UMUHIMU WA IMANI

Katika maisha yetu tunavyo vitu tunavyothamini kuliko vingine kulingana na umuhimu wa vitu vile katika maisha yetu. Hii ni baada ya uchunguzi na upelelezi wa kina sana na hivyo basi mtu aweza kuwa na Imani na kile chombo au kitu

Lakini hapa Paulo atufunza Imani ilivyo maana Zaidi nasoma sasa kutoka waraka wa Paulo kwa Wagalatia 3:26-29

26 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.

27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.

29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Fungu hili latuonyesha faida au Baraka tulizonazo kwa sababu ya kumwamini yesu kristo ya kumwamini yesu kristo nahivyo twaliona na kuupata umuhimu wa Imani yetu katika kristo yesu

1 kwasababu ya kumwamini Yesu kristo sisi tu wana wa mungu, injuli ya yohana 3:16

Kwa maana jinsi hii mungu aliuumbu ulimwengu ili kila amwaminiye asipotee bali aupate uzima wa milele

Tuano uzima wa milele kwa Imani katika yesu kristo

Injili ya yohana 1:12

Bali wote waliokea uwezo wa kufanyika watoto wa mungundiowale waliaminio jina lake

Baraka za Imani katika yesu kristo mwana wa mungu

2 katika kristo yestu wote tunaomwanini tumekuwa mmoja naye mungu mwumba wambingu nan chi ndiye bab wetu hakuna myahudi wala myunani sote tu viungo vya mwili mmoja wa kanisa lake kwahiyo sote tu ndugu na dada kwa Imani katika yesu kristo sasa n ahata milele hii ni Baraka teule

3 kwa sababu ya kumwamini yesu kristoukweli huu yesu kristoukweli huu umedhibitishwa pia katika waraka wa Paulo kwa warumi 8:16-17

16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

Na katika waraka wa Paulo kwa waefeso Paulo aliwaandikia waefeso 1:10-12

10 Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;

11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.

12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.

Na tumshukuru na tumtukuze mungu kwa Imani katika kristo tumekuwa mmoja kanisa lake haijalishi kabla au rangi

Kumwamini yesu tumepewa uweza wa kufanyika watoto wa mungu naye mungu baba ndiye baba yetu wa mbinguni weka Imani yako katika kristo