Maisha Huru

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Maisha Huru
/
Warumi 6:14-23

Hujambo msikilizaji wangu naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha matumaini, leo twalichambua fungu l neno waraka wa paulo kwa warumi 6:14-23. wimbo alfu tuendelee

wimbo

naam karibu tena, Warumi 6:14-23 maisha huru

nchi nyingi huwa katika bara hili la afrika zilipigania uhuru kutoka tawala miliki za wakoloni na ubeberu. Katika nchi yetu ya Kenya nalikuwa kijana wa shule ya msingi na niliona mashujaa wetu walivyoteseka na kunyanyaswa wakipiga vita vya uhuru. Mnamo mwaka 1963 tukanyakua uhuru na baba wa taifa hili hayati mzee Jomo kehyatta alikuwa anasema, yeyote atakayechezea uhuru wetu, yeyote akileta nyoko nyoko ataona cha mtemakuni. Tangu jadi watu hutamani kuwekwa huru lakini kanuni za Maisha zispozingatiwa uhuru waweza kutatanisha. Twajua kiroho tumewekwa huru lakini twahitaji maagizo ya kiroho yaliyo katika neno la mungu. Naam basi nasoma Warumi 6:14-23

14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.

15 Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!

16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.

17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;

18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.

19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.

20 Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki.

21 Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.

22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.

23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Sisi wakristo tumewekwa huru kwa neema yake mungu siyo kea matendo yetu tusije tukajiona na hiyo maana ya kuokolewa kwa neema.

Kwa hiyo Hakuna mtu anayepaswa kuringa eti ni mwongofu kujivuna kwetu kuwe katita utukufu wakekwa neema sisi tumewekwa huru katika kristo hii kwamba hatupaswi kuwa watumwa wa dhambi laikini eti kwa sababu kwa neema tumeokolewa na utumwa wa dhambi tuendelee kutenda dhambi? Kwa neema yake mungu tumepata uhuru lakini haituruhusu kuendelea kutenda dhambi kwa sababu imetolewa mstari wa 16

16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.

17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;

Tukataswa takapata tumaini na tukaheabiwa haki na kufananishwa naye mungu aliye tumaini letu la uzima wa milele. Lakini wanaomkataa yesu na kukataa kumwamini waendeleea kutenda dhambi. Mshahara wa dhambi ni mauti lakini karama ya mungu ni uzima wa milele