Namna Imani Hufanya Kazi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Namna Imani Hufanya Kazi
Loading
/
Warumi 4:19-25

Salaam msikilizaji mpendwa ni wakati wa kujifunza neno la mungu. Leo rwalichambua neno la mungu; waraka wa Paulo kwa warumi 4:19-25 namna Imani hufanya kazi. Jina langu ni david mungai, karibu wimbo halafu tuendelee

Wimbo

Kaributena ,sikilizaji

Kila mmoja kila siku huamua kufanya au kutenda mabo mengi tena tofauti. Unaamua kuondoka kulala, kwenda kazini na kadhalika. Lazima tuamue na kuchagua. Mara twa chagua mema nyakati nyingine mabaya. Baba yetu ibrahimu aliamua kuwa na uchaguzi na mtume Paulo aliandika kuhusu uchaguzi ibragimu alifanya waraka wa Paulo kwa warumi 4:19-25, nasoma

19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.

20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;

21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.

22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

23 Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake;

24 bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;

25 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki

Kila mtu kila siku, kila saa lazima na sharti tufanye uamuz. Twaishi tukiamua kufanya mema au kinyume. Twaamua kuzungumza na mtu akinuna huamua kunyamaza. Twaamua leo, kesho twapata matokeo na kama tunavyoamua ya kimwilii ndivyo nay a kiroho

Na tunapoamua na kufanikiwa kupata mema twapata pumziko.

Baba yetu ibrahimu aliamua maamuzi mengi na mengine yatuhusu sisi kiikani ili tuwezu kuyaelewa ya kiroho kwa mfano, katika kitabu cha mwanzo15 twasoma habariza ibrahimu alivyo mwamini mungu hata kabla ya kutahitiwa kwake. Kutahiriwa kumependekezwa na madaktari, kwa maana ni afya njema, lakini wokovu sisi huupata kwa kumwamini Yesu krristo na kumpokea moyoni.

Ibrahimu alipumzika moyoni akisadiki kuwa aliyoyaahidi mungu atayatimiza. Ni jambo la kustaajabisha namna Imani tuliyo nayo I katika mwenyezi mungu muumba wa mbingu nan chi na ndiye mwenye uweza wote. Mstari wa 24-25

24 bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;

25 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki

Huo ndio mpango wa mungu na mpango huo hukamilika mtu anapomwamini Yesu kristo. Tunapompenda yesu basi uamuzi wa sahihi hupitia kwa Imani yetu tunaomwamini Yesu ni uamuzi uletao kuhesabiwa haki mungu hutusamehe dhambi zetu na kutufanya wapya katika dhamiri moyoni na akili

Yu heri anayeamua kumwamini Yesu maana hiyo ndiyo hali njema na nzuri moyoni. Nakuomba utilie maanani ukweli huu

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!