Kiburi Kujipenda

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Kiburi Kujipenda
Loading
/
I Wakorintho 4:6-9

Hujambo. Karibu tujifunze Neno pamoja. Jina langu ni David Mungai. Leo twalichambua fungu la Neno kutoka 1 Wakorintho 4:6-9 ‘KIBURI’. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena. Siku moja, mmoja wa mwandishi alimwendea Bwana Yesu, akamwuliza “Amri gani ya kwanza?” Bwana Yesu akamjibu akamwambia, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na nguvu zako zote na akili zako zote Mwandishi akasikia kuwa hayo ni mema lakini hakufurahi alipoambiwa na Bwana Yesu ya kwamba, Amri ya pili ni sawa na ya kwanza. Bwana Yesu akamwambia,

“Na umpende jirani yako unavyojipenda. Twajipenda kweli Paulo atuonya kwa maneno yanayopatikana katika Warumi 12:3

“Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunai bali awe na nia ya kiasi kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.”

Neno la Mungu halifundishi tukose kujiheshimu na kujinia mema, lazima tuelewe na kufahamu linavyosema Neno. 1 Wakor 4:6-9.

6 Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa, ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.

7 Maana ni nani atakayepambanua na mwingine? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini? Kana kwamba hukupokea?

8 Mmekwisha kushiba mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam laity mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi.

9 Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho kama watu waliohukumiwa wanawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na kwa wanadamu.

Ili tuweze kujisifu kwa njia inayofaa, kunayo mambo kadhaa tunaopaswa kujua. Lazima tukumbuke kwamba tumo ndani ya mwili wa Yesu Kristo, na viungo vyote sharti na lazima vifanye kazi pamoja na kwa undugu. Tusome tena maneno ya mstari wa 6 na 7.

“Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yalioandikwa, ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.”

7 Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea wajisifia nini kana kwamba hukupokea?

Kwa kifupi Paulo asema, mimi na Apolo tu watu tofauti. Kiwango change cha kuelewa Neno ni cha Apollo, lakini hakuna cha kujivunia maana yote tuliyo nayo kimaumbile na hali, ni vipaji vyake Mungu na kwa neema yake Mungu. Badala ya kujifunza twampa Mungu sifa na utukufu. Ndiyo sababu Paulo auliza. Iwapo ulipokea wajisifia nini kana kwamba hukupokea?

Katika injili ya Marko 9, mitume wa Bwana Yesu walikuwa wanawazawaza, nani akashika usukani, Yesu akaondoka.

Yesu, maana ni Mungu Muumba wa mwanadamu, alijua, aliyasoma mawazo ya mitume, akawaambia: Mst 35 “…Akaketi chini, akwaita wale thenashara akawaambia mtu atakaye kuwa wa kwanza, atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.”

Ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini ulichokipokea? Lakini iwapo ulipokea wajisifia nini, kama kwamba hukupokea?

Hamna sababu kutosha ya kiburi majivuno na hata maringo. Sisi ni mmoja katika Yesu Kristo.
Mst 8 “…Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri mmemiliki pasipo sisi. Naam, laity mngemiliki ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi!”

Yote tuliyo nayo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ameturuhus kumiliki kama mabalozi, na wakili wake. Mwili, akili, na hali mali na fedha tulizo nazo ni mali yake Mungu na ni muhimu na lazima tuzitumikishe kwa unyenyekevu na kwa utukufu wake Yesu. Tosheka na ulicho nacho.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!