Wenye Hekima Hupumbazika

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Wenye Hekima Hupumbazika
/
Warumi 1:18-22

Hujambo na karibu jina langu niDavid Mungai. Leo twalichambua neno la Mungu kutika kitabu cha Warumi 1:18-22. Wenye hekima wapumbazika. Wimbo halafu tuendelee

Wimbo

KARIBU TENA. WARUMI 1:18-22, ni vigumu kutekeleza jambo lolote iwapo tunao wajibu na ujuzi wa kuwajibika hamna kwa kifupi ni kusema, kea mfano una jambo flani la kufanya lakini hauna namna au ujuzi wa kulifanikisha lile jambo kwa mfano wataka kusafiri kutoka mahali flani na njia hamna, unayo hekima wajua lakini wapumbazika.

Nasoma fungu hili la neno waraka wa Paulo kwa Warumi 1:18-22

18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli usijulikane.

19 Kwa maana, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao; maana Mungu mwenyewe ameyadhirisha.

20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!

21 Ingawa wanajua kuna Mungu, lakini hawampi heshima anayostahili, wala hawamshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao tupu zimejaa giza.

22 Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu.

Namna gani wenye hekima hupumbazika?

Wenye hekima hupumbazika kwa kuipinga kweli kwa uovu wao wajua ukweli ila hufanya kinyume. Kwa mfano,

Mwizi hujua ukweli kwamba ni dhambi kuiba mali au kitu kisichokuwa chake na hutua akili yake kuiba

Wajua ukweli na watumia akilizako kuipinga kweli kwa kupamga mambo ya uovu

Wenye hekima hupumbazika kwa uzushi wao mioyo yao ikatiwa giza.

21 Ingawa wanajua kuna Mungu, lakini hawampi heshima anayostahili, wala hawamshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao tupu zimejaa giza.

Wenye hekima hupumbazika wanapojua ukweli lakini kwa sababu ya wivu waomakusudi huwapotosha wengine na wanpofanya hivyo wao wenyewe hupumbazika.

Wajua yesu ndiye njia na kweli na uzima waamini hivyo lakini watangaza kinyume labda kwa radio yako binafsi. Kwa mfano wajua yakwamba mtu akitubu dhambi zake, damu ya yesu huosha zote lakini wewe wapotosha watu kwa kudai kwamba lazima walipe ada Fulani ili dhambi zake ziondolewe. Wapotosha watu wanapo badilisha utukufu wa mungu na kuweka kwa vitu alivyo umba.

Maneno ya Warumi 1:22-23 yaweka huru ukweli huu

Wakijinena kwa wenye hekima walipumbazika 23wakubadili utukufu wa mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu nay a ndege nay a Wanyama na wa vitambaavyo.

Ukweli ulio kweli hupatikana katika neno la mungu lililo hai. Twa litafakari neno na kulijua kwa Imani na ndilo hutuongoza a kutuelekeza mbinguni. Naomba tuwe watu wenye hekima ambao huzingatia ukweli wa neno la ungu na ukweli wa neno utuelekeza na kuthibitisha ya mbinguni.