Ulimwengu Wangoja Kwa Hamu Utukufu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Ulimwengu Wangoja Kwa Hamu Utukufu
/
Warumi 8:18-27

Hujambo na karibu jina lagu ni David mungai, leo katika matumaini twalichambua neno la mungu kutoka Warumi 8:18-27, twangoja utukufu wa mungu kwa hamu. Karibu wimbo halafu tuendelee

Wimbo

Naam karib tena, twalichambua neno kutoka waraka wa Paulo kwa warumi 8:18-27 twangoja utukufu kwa hamu. Utukufu humpa mtu tumaini la kutegemewa twasubiri kwa hamu. Nasoma

18 Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.

19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.

20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;

21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.

22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa.

23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

24 Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?

25 Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Katika fungu hili, Paulo atoa dhihirisho kadhaa zinazoonesha kweli viumbe vyasubiri utukufu

20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;

21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.

22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. Kilicho cha utukufu huo chaendnelea kutamkwa

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Twalia pamoja na Paulo tukisubiri kwa hamu utukufu wa bwana, mahali ambapo twawekwa kutokana na ufisadi na chuki za dunia hii na bwana, katika hii safari ya kwenda mbinguni, alipo bwana ni utukufu tele. Roho mtakatifu ndiye msaidizi wetu