Utawala Wa Sheria

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Utawala Wa Sheria
/
Warumi 7:1-6

Hujambo na karibu, hiki ni kipindi cha matumaini. Leo twalichambua neno kutoka warumi 7:1-6, utawala wa sharia. Jina langu ni david mungai, wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena tujifunze neno la mungu

Kila nchi duniani ina sharia zake. Jamii na makabila hali ni hiyo hiyo. Sharia zimeandikwa. Katika sharia zingine ni zaa kijamii na huzingatia hitikadi mbalimbali duniani na sharia tupu za kumsaidia mwananchi kuishi kwa Amani. Si ajabu kwamba hata katika Maisha ya kiroho mna sheria. Leo twazungumzia utawala wa sheria.

Nasoma neno kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 7:1-6

1 Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati
anapokuwa yu hai?

2 Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.

3 Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.

4 Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.

5 Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.

6 Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.

7 Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.

Sheria inamatakwa yake na mtu hawezi kujiondoa na kama vile mwanamke haruhusiwi na sheria kuoa bwana wake akiwa bado yu hai.

Hii ndiyo sababu neno limesimama ili tuwe huru lazima tukombolewe kutoka kwa sheria nasoma tena maneno ya mstari wa nne

4 Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.

Hatuwezi kuwa nguvu na uweza wetu, hatuwezi kujiondoa kwa nguvu na matakwa ya torati. Ukivunja moja una hatia ya torati yote kwahiyo tunahitaji ukombozi kwa sababu roho zote ni mali ya mungu. Roho ilie itendayo dhambi itakufa. Ezekieli 18:4

Na hatuwezi kupata ukombozi wala nah ii nddiyo sababu kristo alikufa msalabani kwa ajili na kwa niaba yetu sisi wenye dhambi. Ukombozi tu waweza kupatikana kwa kumwamini bwana wetu yesu kristo maana kwa kifo chake mwalabani tulipata njia ya wokovu kwa niaba yetu kristo aliyakamilisha matakwa yote ya torati na sheria