SIMAMA WIMA

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
SIMAMA WIMA
Loading
/

MATUMAINI PROG 1496
TITLE: SIMAMA WIMA
TEXT: WAGALATIA 2:1-5
Hujambo msikilizaji na karibu tujifunze neno pamoja leo twalichambua neno pamoja kutoka wagalatia 2:1-5 jina langi ni David Mungai wimbo alafu tuendelee
WIMBO
Naam karibu tena fnzo letu la leo linapatikana na kutoka wagalatia 2:1-5 kinyonga hubadili rangi ya ngozi kulingana na kuambatana na mazingira yaliyomo na kwa njia huyo hujificha na adui zake watu wengi ni kama kunyonga Imani zao hutegemea mazingira na maslahi ya mtu lakini sharti lazima tusimame imara katika Imani . tusimame wima. Nasoma wagalatia 2:1-5

2 Kisha, baada ya miaka kumi na minne, nilikwenda tena Yeru salemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito ili awe pamoja nami. 2 Nilikwenda kwa sababu nilikuwa nimefunuliwa na Mungu, kwamba nikawaeleze kwa faragha wale waliokuwa viongozi, Injili ninayohubiri kwa watu wa mataifa mengine. Nilifanya hivyo ili kazi yangu niliyokwisha fanya na hii ninayofanya sasa isije ikawa bure.3 Hata hivyo Tito ambaye alikuwa ni Mgiriki, hakulazimika kutahiriwa. 4 Lakini walikuwepo ndugu wengine wa uongo ambao walikuja kwa siri kupeleleza uhuru tulio nao katika Kristo Yesu, ili waturudishe kwenye utumwa wa sheria. 5 Sisi hatukukubaliana nao hata kidogo ili ukweli wa Injili uendelee kutunzwa kwa ajili yenu.

Msimamo wake Paulo ulitokana na kanuni kadhaazilizotawala maisha yake Paulo alihakikishaya kwamba alikuwa sahihi na hakika ya kwamba ujumbe wake ulisambaza ukweli wa injili ya bwana yesu nah ii ndiyo sababu miaka kumi na mine baada ya kuokolewa na yesu alienda yerusalemu apate kushauriana na mitume wengine kama petro pamoja na hayo alisafiripamoja na ndugu wengine barnabas na tito ilia pate kushauriana nao
Ni vyema na ni muhimu kushauriana na nfugu katika huduma zetu
Kanuni ya pili Paulo alisimamia haki yake hakubadilisha msimamo wake wala ujumbe wake kulingana na mazingira wala maslahi. Paulo hakuzingizia watu wa mataifa watahirirwe kwa sababu ya sharia iyopewa. Waisraeli kwa sababu alimhubiti kristo aliyeikamilisha torati na sharia zote kikamilifu na kwa kumwamini yesu hata wetu waleo huupokea n ahata waleo hiipokea wokovu kamili haijalishi kabisa. Twaokolewa kwa Imani lakini matendo yetu yasiende kinyume na maagizo ya neno la mungu kwa viongozi wa roho mtakatifu ni injili moja ya wokovu kwa kumwamini yesu kwa mataifa yote wa rangi yote bila ubaguzi
Paulo alisema hayo kwa himizo katika sura ya kwanza ya wataka huu mstari wa 8-9
Lakini kuwa sisi au malaika wa mbingu atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria na alaaniwe
Kama tulivyotangulia kusema na sasa nasema tena mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyopokea na alaaniwe
Paulo alihikisha yakwamba aliyohubiri na kweli namna gani aliomba alikuwa na uhusiano mwema na yesu bwana na mwokozi na pia alishauriana na mtume na ndugu wengine katika kristo
Paulo alisemama wima katika kumwamini na kumtumikia bwana na mwokozi yesu kristo. Hakubadilishwa wala kushawishiwa na mazingira na hali mbali mbali kwa wote aliwapa habari za wokovu katika kristo zkwa himizo la kumpokea yesu kristo
OMBI
Endapo wahitaji msaada Zaidi rafadhali wasiliana nasi. Anwani na nambari zetu za simu ntakusomea baada ya wimbo huu
WIMBO
MATUMAINI
TWR
SLP 21514-00505
NAIROBI KENYA
SIMU: 0721970520
BARUA PEPE: [email protected]

Jina langu ni david mungai, kwaheri kwa sasa.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!