SHERIA NA INJILI

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
SHERIA NA INJILI
Loading
/

MATUMAINI PROG 1492
TITLE: SHERIA NA INJILI
TEXT: WAGALATIA1 1:1-5

Hujambo msikilizaji wangu mpendwa, jina langu ni david mungai na ni futaha yangu kukuletea kipindi cha matumaini. Leo twalichambua fungu la neno kutoka waraka wa pailo kwa wagalatia 1:1-5, sharia ndani ya injili. Wimbo alafu tuendelee

WIMBO
Naam karibu tena tujifunze neno pamoja waraka wa Paulo kwa wagalatia 1:1-5 sheria ndani ya injili
Mungu huchagua kuwarumia watu katika mpango na utaratibu wake na hivi watu wengine wamejitangaza kuwa watumishi wa mungu lakini makundi na mathumuni yao ni yao wenyewe binafsi n ahata wanapohutubu hutia hituba zao wenyewe na kwa manufaa yao wenyewe swali ni kwamba twawezaje kuwa walio na wasio kweli? Tutalipata jibu katika fungu hili la neno. Nasoma wagalatia 1:1-5

Mimi Paulo niliye mtume si kwa mamlaka ya binadamu, wala si kwa nguvu ya mtu, bali kwa uwezo wa Yesu Kristo na wa Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu, na ndugu wote walio pamoja nami tunayasalimu makanisa ya Galatia. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba, ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu mbaya wa sasa. Kwake yeye uwe utukufu milele na milele! Amina.

Mwandishi wa waraka huu kwa wagalatia ni Paulo aliyekuwa amepewa jina sauli na wazazi wake walimcha Mungu wazazi wake walikuwa wayahudi wa kabila la benjameni na mfalme sauli alikuwa wa kabila moja na Paulo sauli ni jina la kiebrania lakini alipmwamini Yesu alipewa jian la kigiriki ma ndiye mwanzilishi wa kanisa la galilaya
Wito wake Paulo haukutokana na bidi za kibinadamu bali ni mungu. aliitwa na mungu na aliwaita wakristo wagalatia, ndugu
Tazama maneno ya mstari wa kwamza ma wa pili hatakama wagalatia walikuwa watu wa mataifa katika kristo yesu Paulo awaita ndugu katika kristo. Sote bila ubaguzi wa rangi, taifa au kabila sisi ni ndugu na undugu wetu ni wa kudumu ilele na milele haijalishi ndugu yako ametoka dunia ipi
Nakumbuka siku moja mimi na mwenzangu mch stepeni tulikuwa shuttigart uwanjani tulilakiwa kuhutubu kuhusu huduma ya TWR. Tulipewa dakika tano tu za kuhutubu. Baada ya hayo mama mmoja mzee alikuja niliposiama akaniambia kwamba yeye ni mjerumani lakini yeye huwasaidia ndugu kaitika kristo kwa maombi na msaada wa kifedha katika bara la Afrika bika ubaguzi
Wakati ule wajerumani wa mashariki hawakuruhusiwa kushirikiana na wa magharibi kwa sababu ya tofauti za kisiasa
Mama alikuwa anaenda kwa daktari wa meno na kujazwa mawe ya dhahabu almasi n ahata fesha alipotembea wejerumani wa magharibi alitolewa yale mawe na kuyapeleka ofisi zetu za ERF na kuwapa wauze apate kuwasaidia ndugu katika bara la Africa kwa sababu ya undugu katika kristo ni muhimu tujue na kufahamu ya kwamba kamailivyokuwa na Paulo yapaswa kuwa vivyo hivyo
Pamoja na hayo Paulo aliwaombea ndugu wagalatia undugu wa ukristo ni wa kuombeana pia rukukumbushana umuhumu wa kumshukuru mugnu kwa kumtoa mwanawe wa pekee yesu kristo awe mwokozi wetu, mkombozi wa nafsi zetu huyu Bwana ndiye ametuokoa kutika kwa dhambi na nguvu zake na kutuingiza katika zizi la wale watakaourithi ufalme wa wa milele katika kristo bwana wetu Yesu kristo aliyekamilisha matakwa yote ya sharia na kwa neema yake na kwa kumwamini tumehesabiwa haki na tumekuwa warithi wa mji wa mbinguni. Bwana aita bila ubaguzi
OMBI
Endapo wahitaji msaada zaido, tafadhali wasiliana nasi. Anwani na nambari zetu za simu ntazisoma baada ya wimbo huu

WIMBO

MATUMAINI
TWR
SLP 21514-00505
NAIROBI KENYA
SIMU 0721970520
BARUA PEPE: [email protected]
Jina langu ni david mungai, kwaheri kwa sasa.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!