Mahali Petu Katika Mpang Wa Mungu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mahali Petu Katika Mpang Wa Mungu
Loading
/
Wagalatia 4:4-7

Hujambo msikilizaji mpenzi wa kipindi hiki cha matumaini, leo twalichambua fungu la neno kutoka waraka wa Paulo kwa Wagalatia 4:4-7, mahali petu katika mpango wa mungu. jina kangu ni David Mungai, karibu wimbo alafu tuendelee

Naam karibu tena, waraka wa Paulo kwa Wagalatia 4:4-7 MAHALI PETU KATIKA MPANGO WA MUNGU

Katika tamaduni kunao baadhi ya makabila ambao walitumia mbuzi au kondoo kuwapokwa watoto ambao hawakuzaliwa katika boma aufamilia, walitoa mbuzi au kondoo kumchunga halafu yule mtoto kuzaliwa mle na hivyo ndivyo Paulo anajaribu kuwaeleza wagalatia kwamba walizaliwa katiak ufalme wa Mungu, kondoo wa mungu, yesu kristo nasoma fungu hili na neno

4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,

5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.

6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.

7 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.

Ili kuhakikisha ya kwamba sisi watu wa wanadamu tumezaliwa upya katikafamilia ya wana wa mungu, mungu alituma mwanawe wa pekee kondoo wa mungu aichukuaye ndambi ya ulimwengu aimwagaye damu yake msalabani ili kwa damu hiyo ailipe fidia, tupate ondoleo la dhambi na kuzaliwa upya katika familia ya mungu katika familia ya mungu kama watoto wake. Tumepata uwezo wa kuitwa wana wa mungu

Tumezaliwa na mama zetu tukiwa wenye dhambi lakini kwa damu ya ysu tumezaliwa kuwa wana wa mungu

Pamoja na hayo mungu baba alimtuma bwana wetu yesu kwa kifo chake tupate ondoleo la dhambi na tuna weza kufurahia na kusherehekea kuzaliwa katika familia ya mwenyezi mungu na kama wana tuna fuhusa na ueza wa kumwendea baba yetu mbibnguni ba haja na mahitaji yetu baba hawezi kumnyima mwana chochote ambacho ni kizuri ni furaha ya mzazi kumtunza mwana hata kama hujui kuomba ni vyema kujua ya kwamba bwana yesu na roho mtakatifu hutuombea

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe hapaduniani kama ilivyo mbingu, utupe leo riziki yetu,
Utusamehe makossa yetu kama tumavyo wasamehe wanao tukosea,
Kwakuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu sasa n ahata milele
Amen

Hivyo ndivyo tunavyopaswa kuomba pamoja na hayo neno lasema Roho mtakatifu hutuombea mbinguni warka wa Paulo kwa warumi 8:26-27

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Kwa upendo mwingi mungu ametufanya wata, warithi wa mji wa mbinguni milele na milele Amina

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!