NJIA YAKIPEKEE NA YA KWELI

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
NJIA YAKIPEKEE NA YA KWELI
Loading
/

MATUMAINI PROG 1493
TITLE: NJIA YAKIPEKEE NA YA KWELI
TEXT: WAGALATIA 1:6-9
Hujambo msikilizaji wangu natumai ubuheri wa afya na hilo ndolo ombi langu. Leo twalitazama kwa wimbo alafu tuendelee

WIMBO

Naam karibu tena waalatia 1:6-9 ndilo fungu letu la leo . kunazo dini nyingi sana duniani na kila dini huwa na mafundisho yake na kila dini hufuata njia za kumfikia mungu
Twaamini kunayo mbinguni na mwenyezi mungu ndiye mwenyeji na kwasababu yeye si mchoyo ametupatia njia inayotuelekeza huko aliko na hiyo njia ni kuupokea ukweli wa injili ya bwana wetu yesu kristo nasoma kutoka waraka wa Paulo kwa wagalatia 1:6-9
 
Nashangaa kuona kwamba mnamwacha upesi hivyo yule aliye waita kwa neema ya Kristo mkaanza kufuata Injili nyingine. 7 Ukweli ni kwamba hakuna Injili nyingine, ila nafahamu kuwa wako watu wanaowavuruga, ambao wanataka kuipotosha Injili ya Kristo. 8 Lakini hata ikiwa ni sisi au ni malaika atokaye mbinguni, kama mtu akiwahubiria Injili ambayo ni tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo na alaaniwe. 9 Kama tulivyokwisha sema kabla, sasa nasema tena, kwamba mtu ye yote atakayewahubiria Injili tofauti na ile mliyokwishaipokea, basi mtu huyo na alaaniwe.

Kutoka kwa fungu hili la neno la mungu Paulo atunyesha kweli kadhaa zinazotuonyesha injili ya bwana yesu ndiyo injili pekee ya ukweli
Ukweli ni kwamba injili ya kweli yatokana na bwana wetu yesu kristo. Yesu kristo ndiye kigogog na msingi wa injili . habarinjema ya wokovu
Nastaajabu kuwa mnamwacha upesi hivi aliyewaita katika neema ya kristo a kugeukia injili ya namna nyingine
Injili ya kweli hutoka na imetoka kwa yesu kisto maana ndiye kweli
Ukweli wa pili kunayo injili ya kweli katiak mstari was aba twapata maneno haya
Wala si nyingine lakini wapo watu wawaraabishao na katika kugeuza injili ya kristo
Na njia ya pekee yakuijua na kuifahamu injili iliyogeuzwa ni kuijua sana injili ya kweli na sahihi ukijua kweli dahihi na kweli itakuwa rahisi sana kujua injili ya uwongo kwa mfano wanaotuhudumia katika banki zetu hufunzwa sana namna yakuijua noti au sarafu iliyokweli na katika harakati hizo huijua anapoiguza kwa mikono yake hii kuwa ikuugusa ya uongo haga kikiwa giza ataijua tu. Na hivyo ndivyo ilivyo ukijua injili ya kweli injili ya bwana wetu yesu kristo kwa Imani na kulisoma neno na kulitafakari maramoja utaijua injili ya wongo.
Roho mtakatifu wa mungu atakukumbusha ukweli wa neno lake. Lichambue neno upate kujua ukweli wa injili
Ukweli wa tatu neno la mungu laeleza ilivyo injili ya kweli injili ya kweli itamhubiri kristo
Injili ya kweli twapata kwa kumwamini Yesu Kristo na kumkiri na matendo na vinywa vyetu
Injili ya kweli hutenda Amani moyoni maana hutupa uhakika kwambatumesamehewa dhambi zetu
Injili ya kweli ni kwa neema wala si kwa matedo yetu
Paulo alihubiri injili mabayo kweli amna mtu awezaye kuigeuza waka kuibadili
OMBI
Endapo wahitaji msaada Zaidi tafadhali wasiliana nasi. Anwani na nambari ya simu ntazisoma baada ya wimbo huu
WIMBO
MATUMAINI
TWR
SLP 211514-00505
NAIROBI KENYA
SIMU 07211970520
BARUA PEPE: [email protected]
Jina langu ni david mungai, kwaheri

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!