Rafiki Wa Karibu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Rafiki Wa Karibu
/
Isaya 53:1-6

Hujambo na karibu. Wakati umewadia, wakati wakujifunza neon la mungu. Leo twalichambua neon kutoka chuo cha nabii Isaya 53:1-6, rafiki wa karibu. Jina langu ni david mungai. Wimbo alafu tuendelee na safari yetu.

Wimbo

Naam karibu tena chuo cha nabii Isaya 53:1-6

Wakati mmoja, mmoja wa rais alikuwa hatarini. Mmoja wa adui zake alimlenga risasi lakini haikumpata kwa sababu askari wake mlinzi aliingia kati ili risasi impate ingawa hakufa lakini alimwokoa rais. Rahis yule alimshukuru sana askari yule na wakawa marafiki wa karibu.

Katika fungu hili la Isaya 53:1-6 twasoma rafiki yetu wa karibu yesu kristo maana ndiye aliyeingia kati yetu na kifo cha milele katika bahari ya moto.

1 Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.

3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

Katika mstari wa kwanza wa fungu hili isaya 53:1 maswali kadhaa yameulizwa.

Ni nani aliye iandika habari habarituliyoileta?

Maswali hayo yadokeza kuwasio wengi walimjua na kumfahamu rafiki wa karibu kwa maana tumwonapo hana uzuri n ahata umbo hakuwa nalo. Je, huyu alikuwa nani? Kama anavyoelezea katika neon hili. Huyu rafiki wa karibu ni yesu.

Ni yesu aliyedharauliwa na watu bila sababu. Alikataliwa na wengi, mtu wa huzuni na ajuaye masikitiko. Alidharauliwa wala hatukumhesabu kwa kitu. Na kwa sababu ni rafiki wa karibu neon lasema, 4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Pamoja na hayo yesu kristo akatutengenezea njia ya kuturejesha kwake. Kila wakati maana bado twaishi kwatika dunia telezi twaanguka. Tunapotenda dhambi katika hisia zetu, na kwa matendo yetu lakini neon limetuhakikishia kwamba Bali alijeruhiwa kwa makossa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya Amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.mlango bado uwazi kwa yeyote anayetubu na kuungama dhambi zake.

Na sikiliza habari njema, ‘na bwana ameweka juu yake, maovu yetu sisi sote.

Lakusikitisha ni kwamba katika kitabu cha ezekieli 18:4,

Tazama roho zote ni mali yangu, kamavile roho ya baba ni mali yangu ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu. Roho itendayo dhambi itakufa.

Tubu ungama, kiri dhambi zako na utakuwa na uhusiano mwema na wa karibu na bwana Yesu aliyejitoa kwa ajili na kwa niaba yetu na maisha yetu.