Mungu Ni Wa Kweli

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Ni Wa Kweli
Loading
/
Isaya 65:17-25

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha matumaini na twalichabua neno kutoka chuo cha nabii Isaya 65:17-25, mungu wa kweli anaposhika ususkani. Jina langu ni david mungai. Sikiliza wimbo alafu tuendelee.

Wimbo

Karibu tena tulichambue neno la mungu kutoka chuo cha nabii Isaya 65:17-25. Katika fungu hili la neno la mungu, twamwina mungu kazini.

Mungu ndiye muumba w vitu vyote, ndiye hudumisha vyumbe vyake vyote. Na ndiye amefanya binadamu kumwakilisha dunani humu kama tunavyosoma katika kitabu cha mwanzo. Na sema kwamba mwanadamu ndiye atatawala manyama wengine wote, lakini shetani mwongo amejifanya kuwa bado ndiye amiliki na atamiliki. Nasoma fungu hilo la neno, chuo cha nabii Isaya 65:17-25

17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.

18 Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha.

19 Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.

20 Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.

21 Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake.

22 Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.

23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao.

24 Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.

25 Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana.

Kweli itakuwa furaha tele Mungu atakapo shika usukani wa mambo yote katika ufalme wa bwana Yesu wa miaka elfu.

Na kwa sababu kutakuwa na mabadiliko, furaha isiyo kifani itakuwepo katika ufalme wa kristo. Tuangalie tena neno mstari wa 18 Lakini furahini, mkashangilie daima…

Na katika agano jipya yohana mwandishi wa kitabu cha ufunuo akubaliana na kuweka nguvu ukweli huo ufunuo 21:4 naye atafuta kila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwepo tena, wala maomhplezp wala kilip wala maumivu hayatakuwepo tena kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Mungu ataumba uhai mpya motto atakuwa motto akiwa na umri wa miaka mia. Watu watajenga nyumba na kupeana mwigine akae… na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.

Utakuwa utawala wa amani maana mfalme wa wafalme na amani atakuwepo…popote alipo yesu huwa na amani tele na hili ndilo tumanini letu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!