Mikono Ya Mungu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mikono Ya Mungu
Loading
/
Isaya 40:10-15

Hujambo naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi cha kujifunza neon la mungu Matumaini. Leo twalichambua neno la mungu kutoka isaya 40:10-15. Wimbo alfu tuendelee.

Na karibu tena tujifunze neno kutoka chuo cha nabii isaya 40:10-15, mikono ya mungu.

Nabii isaya aliishi wakati taifa la waisraeli lilikuwa limeacha kuzingatia maagizo yake mungu utabiri wake uliwalemga sana waisraeli. Waisraeli walivutiwa walikuwa na mvuto wa kuabudu sanamu kama majiani zao.

Ili awarejeshe waisraeli katika njia zake mungu alitumia isaya na ujumbe uliowakumbusha waisraeli kwamba mungu, muumba wa mbingu na nchi ni mkuu mwenye uweza na nguvu kuliko miungu ya sanamu. Nasoma sasa fungu hili la neno la mungu isaya 40:10-15

10 Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.

11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

12 Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?

13 Ni nani aliyemwongoza roho ya Bwana, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake?

14 Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonyesha njia ya fahamu?

15 Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.

Kweli mkono wa mungu una uweza na nguvu zote. Katika mstari wa kumi na tano nasoma tena,

15 Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.

Duniani tuna nchi 195 au mataifa 195. Unapotumbukiza ndoo ya maji mtoni au baharini, kuchota maji unapoiondoa ole ndoo majini kunayo matone ya maji hudondoka.mataifa yote duniani, kwake mungu ni kama Tone la maji mkononi mwa mungu mna uweza na nguvu zote na kweli anastahili heshima zote na ibada zetu zote.

Jambo au ukweli mwingine tunapata kutoka fungu hili la neno ni kwamba mungu aliumba vyote kwa uadilifu sahihi kabisa.

12 Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?

Bwana azimiwe, dunia na viumbe vyote aliyafanya bwana mungu ndiye bwana wa mabwana.

Jambo la tatu, Mungu hutawala kwa nguvu na uweza wa mikono yake kama tunavyosoma katika mstari wa 22 na 24 wa sura hii

22 Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;

24 Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi
katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.

Jibu; hakuna wa kufananishwa naye mwenyezi mungu.

Ndivyo sababu mwandizhi wa zaburi alisema, zaburi46:1;

Mungu wetu sisi ni kimbilio na nguvu na msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Pamoja na hayo, mungu hutoa huduma yake kwa huruma zake za upendo kwa kondoo zake.

11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole

Mungu wetu katika Yesu kristo ni mwingi wa huruma kwetu sisi kondoo zake.

Bwana wetu tukiwa katika mikono yake hututawala na ulimwengu wote pia.

Mungu aliumba vitu vyote kwa uadilifu.

Mungu hutawala kwa uweza na nguvu za mikono yake.

Hakuna wa kufananishwa na mungu wetu katika kristo yesu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!