Mungu Aki Hukumu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Aki Hukumu
Loading
/
Isaya 24:1-6

Hujambo na karibu tujifunze neon la mungu. Kitabu cha Isaya 24:1-6, Munug akihukumu. Jina langu ni David Mungai, wimbo alfu tuendelee

Naam, karibu tena. Leo twalchambua neon la mungu kutoka Isaiay 24:1-6. Nyakati nyingi hasa ule wakati tanapitia mambo magumu na msaumbuko, mara sisi hujiuliza mungu yu wapi? Je,Mungu yupo? Na wakati mwinginetnaanza kulia, mungukama unaisikia tafadhali nisaidie wakati mwingine husahau ya kwamba anayajua yote na ndiye mtawala katika historia yote tangu jadi. Na biblia husema, kila mmoja wetu atasimama mbele ya kiti cha mungu. Mungu pekee ndiye anajua siku hiyo itakuwa lini.

Nasoma sasa kutoka kitabu cha Isaya 24:1-6

1 Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.

2 Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.

3 Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo.

4 Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.

5 Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.

6 Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.

Nabii isaya alionyeshwa na mwenyezi mungu kuomba siku moja ya siku mungu atatoa huumu kwa hiyo isaya atuonya.

Nabii isaya atutolea onyo. Machoni mwake mungu sote tuko sawa, hakuna mwenye mamlaka kuliko mwingine.

2 Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.

Kwa ufupi,twajifunza yakwamba machoni mwa Mungu sote ni sawa vyeo vyote vitaondolewa na hukumu yake mwenyezi mungu. Usimwone mwenzako kuwa si kitu machoni mwa mungu mko sawa.

Mimea yote itaharibiwa Mungu akitoa hukumu, vyumbe vyote hupata madhara na kama vile unamwaga maji au maziwa kutoka kwa kibuyu mpaka tone la mwisho. Hamna cha ziada. Akisema amesema

3 Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo.

Dini haitafua dafu; Mungu atakapoihukumu dunia kwa sababu mpiga kristo atatumia dini, kuyabalilisha maagizo yake mungu. Mungu ataihukumu hiyo dini. Dini zime batlisha maagizo yake mungu na hazitahepuka hukumu yake Mungu. Kunao watu wanaoabudu dini kuliko Mungu. Na hakuna wa au cha kulinganishwa na mwenyezi Mungu. Ninchukizo kwake Mungu kufundisha au kuchukua nafasi yake mungu maishani mwa mtu.

Mungu lazima aabudiwa kama Mungu kwa unyenyekevu na heshima zote. Mungu si sanamu au mawazo. Lazima tumwabudu kwa roho na kweli.

5 Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.

Mungu kwa upendo mwingi na rehema zake ametupatia njia ya kuurejesa uhusiano mwema nay. Njia ya kurejesha uhusiano mwema naye. Nia hiyo ya pekee ni kutubu na kump Mungu mahala pa kwanza maishani mwetu, maana ndiyo njia ya pekee ya kumrudia Mungu Amini na ulitii neon lake.

Pahali urafiki wako na Mungu kwa kumwamini bwana wetu yesu kristo upate tegemeo na ondoleo la hukumu. mshahara wa dhambi ni mauti.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!