Jihepushe Na Hukumu Ya Kifo

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Jihepushe Na Hukumu Ya Kifo
/
Wagalatia 3:10-14

Hujambo mpenzi msikilizaji, natumai ubuheri wa afya na hayo ndiyo maombi yangu. Leo twalichambua neno kutoka kwa waraka wa Paulo kwa Wagalatia 3:10-14, jihepushe na hukumu ya kifo. Wimbo alafu tuendelee

Naam karibu tena tujifunze neno. Twalichambua fungu la neno kutoka kwa waraka wa Paulo kwa Wagalatia 3:10-14 naoma fungu hili la neno

10 Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

11 Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.

12 Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo.

13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

Mwiaho wa somo. Fungu hili la somo kweli laonyesha hali ya kuhuzunusha. Hukumu tayari imetolewa

Hebu tuelewe ya kuwa sharia na torati ilitolewa kutuonyesha utakatifu wa mungu na hakuna mwanadamu anayeweza kutimiza matakwa ya torati na sharia . sharia na torati hufafanua utakatifu wa mungu na kwa matendo yetu hatuwezi kufikia kiwango cha utakatifuwa mungu nasi tuko chini ya laana hatuna nguvu na ushindi hatupati nsaoma mstari wa kumi tena

10 Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa,

Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye

Lakini twaweza kujiepusha na hiyo laana kwa kutubu dhambi zetu zote na kumwamini yesu kristo. katika yesu kristo tumehesabiwa haki na kuishi kwa Imani na katika tumaini la uzima wa milele

Katika kristo laana imeondolewa kaka tulivyosoma katika mstari wa 13

13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

Kristo aliangikwa juu ya msalaba kusudi atuondolee laana ya dhambi kifo cha pili katika bahari ya moto wa milele

Njia ya kujihepusha na kifo hicho ni kutubu dhambi kuungama na kuacha njiaza dhambi na kumpokea yesu kristo kuwa mwokozi na mkombozi wetu