Ibrahimu Alimwamini Mungo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Ibrahimu Alimwamini Mungo
Loading
/
Warumi 4:1-5

Hujambo na karibu. Ina langu ni Dvid Mungai na ni furaha yangu kukukaribisha katika kipindi hiki cha kilichambua neno. Wraka wa Paulo kwa warumi 4:1-5

“IBRAHIMU ALIMWAMINI MUNGU”

Wimbo halafu tuedelee

Wimbo

Naam. Karibu tena,tujifunze neno la Mungu.

Watu wengi katika ulimwengu wa kidini wengi wapenda sana kujihusisha na baba Ibrahimu alikuwa mtu wa vitendo,na kweli alikuwa mtu wa vitendo lakini ni vitendo vya maana gani ? Paulo asema hivi katika

Warumi 4:1-5

1 Basi tseme aje ju ya Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili?

2 kwa maana ikiwa ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake analo la kujisifia lakini si mbele ya Mungu

3 maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwke kuwa haki

4 lakini kwa mtu afanyaye kazi,ujira wake huhesabiwi kuwa ni neema bali kuwa ni deni.

5 lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia imani yake mtu huyo amehesabiwa kuwa haki.

Kutoka kwa maisha ya ibrahimu twaweza kujifunza mafunzo au mambo kadhaa kwa jinsi ya mwili.

Jambo la kwanza hatuna la kujisifia matendo yetu mbele ya Mungu. Matendo,yetu mbele ya Mungu. Matendo kama vile alivyosema isaya ni kama matambala ya nguo chafu mbele zake Mungu. Ni kama zile nguo chafu hutumia kila mwezi na kina mama.

Ni kama kaburi zilizofunguliwa. Harufu mbaya isiyopendeza kwake Mungu. Kwa huyo Ibrahimu hakuhesabiwa haki kwa sababu ya matendo yake bali kwa imani. Mstari wa kwanza . warumi1:1-3

1 “basi tuseme aje ju ya ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili?

2 kwa maana ikiwa ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake analo la. Kujisifia lakini si mbele za Mungu.

3 maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki.

Matendo yake irahimu yalihitaji imani. Alimtoa isaka kwa sababu alimwamini Mungu kwanza. Aliamini kwamba anayosema Mungu sharti yakamilike.maana ukweli wa Mungu lazima udhibitishwena matendo yetu.

Tumesoma katika mstari wa tatu kwamba ibrahimu alimwamini Mungu ili ahesabiwe haki.

Katika kitabu cha mwanzo 15 twapata habari za ibrahimu kwamba Mungu alimahidi irahimu kuwa yeye na sarai watapata motto na hata kwa uzee wake. Walikuwa wamepita umri wa kupata watoto lakini ibrahimu aliamini sarai naye alicheka lakini baadae alijifungu motto wa kiume isaka na likawa taifa la wengi.

Si kwa matendo yake mema bali kwa neema alihesabiwa haki.warumi 4:5

“lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye amaye amhesabia haki asiyekua mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki .”

Imani husababisha kipawa cha neema na chanzo cha neema ni mungu mwenyewe. Na ni kwa neema yake Mungu huleta kuhesabiwa haki.

Basi na tutafute kumwamini Mungu kama ibrahimu tupate kuhesabiwa haki kwa neema yake Mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!