AHADI ZA UTOAJI

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
AHADI ZA UTOAJI
Loading
/

MATUMAINI PROG NO 1476
TITLE: AHADI ZA UTOAJI
TEXT: 2 WAKORINTHO 9:6-15
Hujambo msikilizaji wangu mpenzi na karibu tujifunze neno pomoja. Jina langu ni david Mungai. Leo twalichambua neno la Mungu kutoka kitabu cha 2 wakorintho 9:6-15, AHADI ZA UTOAJI’. KARIBU WIMBO HALAFU TUENDELEE
WIMBO
Naam, karibu tena tujifunze neno pamoja 2 wakorintho 9:6-15 . nasoma
Lakini nasema neno hili apandaye haba atavuna haba. Apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu
7 kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima maana mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu
8 na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa mingi ili ninyi mkiwa na riziki za kila namna siku zote mpate kuzidi sana katika kila tendo jema
9 kama ilivyoandikwa ametapanya amewapa maskini haki yake yakaa milele
10 na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda na mkate uwe chakula atawapa mbegu za kupanda na kuzidisha naye atayaongeza mazao ya haki yenu
11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu
12 maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani ninyi apewazo mungu
13 kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo wanamtukuza mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri injili ya kristo na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote
14 nao wenyewe wakiomba dua kwa ajili yenu wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu
15 Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo
Kwenye maneno ya mstari wa 6 na 11 twapata ukweli kwamba apandacho mtu ndicho huvubna ukweli huu pia umetajwa katika kitabu cha mithali 11:24
Kuna atawanyaye lakini huongezewa Zaidi kuna azuiaye isivyo haki lakini hueleka uhitaji hebu sikiza maneno ya mstari wa nane tena
Na maana aweza kuwajaza kila neema kwa wingi ili ninyi mkiwa na riziki za kila namna siku zote mpate kuzidi sana katika kila tendo jema
Mungu humzidisha mtu Baraka mwenye matendo mema kwa yeyote atoaye kwa moyo mkunjufu mstari wa kumi
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda na mkate uwe chakula atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha naye atayoongeza mazao ya haki yenu
Na hata katika AGANO LA KALE mambo yalikuwa vivyo hivyo. Nasoma hosea 10:12
Jipandieni katika haki vuneni kwa fadhili uchimbueni udongo wa mashamba yrnu kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta bwana hata atakapokuja na kuwanyeshea haki
Ukipenda kupata mavuno ya haki panda katika haki. Acha unyanyasaji na udanganyifu toa kwa moyo mkunjufu
Tukitoa kwa mioyo mikunjufu na kwa haki kipawa cha pesa kitaondoa shida na changamoto za wengi katika shirika na kutoa shukrani. Nasoma mstari wa 12
Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyinyi apewazo Mungu
Kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri injili ya Kristo na kwa ajili ya ukarimu mliowashirikisha wao, na watu wote
14 nao wenyewe wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu
15 Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake tusichoweza kukisifu kama ipasavyo
Wakristo wa Yerusalemu walionea shauku wakristo wa korintho kwa upendo na ukarimu wao. Waliowaombea na kumshukuru Mungu. Na hiyo ndiyo ahadi ya utoaji kwa ukarimu ukifanya hicyo watamtamani na hata kutilia maanani Imani yao katika Kristo bwana na mwokozi wetu. Mungu ndiye anayetuahidi hayo.
OMBI
Endapo wahitaji maelezo Zaidi tafadhali wasiliana nasi. Anwani na nambari yetu ya simu tazisoma baada ya wimbo huu

WIMBO
Matumaini
Twr
SLP 21514 CODE 00505
NAIROBI K X2
SIMU/SMS 0721 970 520 X2
BARUA PEPE : [email protected]
Jina langu ni david mungai
Kwaheri.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!