FURAHA YAKE PAULO

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
FURAHA YAKE PAULO
Loading
/

MATUMAINI PROG NO 1472
TITLE: FURAHA YAKE PAULO
TEXT: 2 Wakorintho 7: 2 – 16

Hujambo na karibu. Natumai u buheri wa afya msikilizaji, na karibu tujifunze Neno pamoja. 2 Wakor 7: 2 – 16. FURAHA YAKE PAULO . Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee
WIMBO
Naam. Karibu tena, tujifunze Neno pamoja.
Nasoma;
2 Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukudhulumu mtu yeyote, wala kumharibu mtu wala kumkaramia mtu.
3 Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi nimo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja na kuishi pamoja.
4 Ninao ujasiri mwingi kwenu, naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha kupita kiasi.
5 Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu, bali tulidhikika kote kote, nje palikuwa na vita, ndani hofu.
6 Lakini Mungu mwenye kuwafariji wanyonge alitufariji kwa kuja kwake Tito.
7 Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidi yenu kwa ajili yangu hata nikazidi kufurahi.
8 Kwa sababu, ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule, sijuti, hata ikiwa nalijuta, naona ya kwamba waraka ule uliwahuzunisha ingawa ni kwa kitambo tu.
9 Sasa nafurahi, si kwa sababu, ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tedno letu katika neno lolote.
10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo, Wokovu lisilo na majuto, bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
11 Maana, angalieni kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu, kulitenda bidi kama nini ndani yenu; naam na kujitetea, naam, na kukasirika, naam na hofu, naam na shauku, naam na kujitahidi, naam na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.
12 Basi ijapokuwa naliwaandikia siku kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake yeye aliyedhumuliwa bali bidi yenu kwa ajili yetu ipate kudhuhirishwa kwenu mbele za Mungu.
13 Kwa hiyo tulifarijiwa. Tena katika kufarijiwa kwetu tulifurahi sana kupita kiasi kwa sababu ya furaha ya Tito, maana roho yake imeburidishwa na ninyi nyote.
14 Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lolote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa, bali kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.
15 Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi akumbukapo kweli kwenu ninyi nyote, jinsi, mlivyomkaribisha kwa hofu na kutetemeka.
16 Nafurahi, kwa sababu katika kila neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu.
Paulo aonyesha furaha kuu sana kwa sababu, Tito alimletea habari njema kuwahusu Wakorintho kama vile tumesoma kutoka mstari wa 5-7, maana tayari Paulo alikuwa amewapelekea Wakorintho barua kali, kwa sababu ya tabia mbaya katika Imani yao. Wakorintho walikuwa walichafua kanisa kwa kiburi na uzinzi nahata ilafu. Paulo akawakemea sana kwa barua, lakini ule waraka ukapotea ndiyo baadaye kaandika waraka huu tunaochambua sasa. Hebu na tusome tena maneno ya mstari wa 5-7:
“5 Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu, bali tulidhikika kote kote, nje palikuwa na vita, ndani hofu.
6 Lakini Mungu mwenye kuwafariji wanyonge alitufariji kwa kuja kwake Tito.
7 Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidi yenu kwa ajili yangu hata nikazidi kufurahi.”
Paulo alijawa na furaha kupokea habari za watoto wake wa kiroho.
Na hapo ndipo sisi tumeanguka. Hatufuatilii kujua hali ya kiroho kwa wakristo wachanga kiimani. Ni jukumu letu, na paswa kuwa, furaha yetu kama ilivyokuwa na Paulo.
Funzo linguine tunalopata hapa ni kwamba, huzuni yao wakorintho, iliwaelekeza kwa toba. Waliyaona makossa yao na kuungama.
Nasoma mstari wa 11:
“ Maana, angalieni kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu, kulitenda bidi kama nini ndani yenu; naam na kujitetea, naam, na kukasirika, naam na hofu, naam na shauku, naam na kujitahidi, naam na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.”
Toba na kujifwalia ahadi zake Mungu, ndiyo njia ya kutusafi mioyo na nashuli zetu.
Zoeza akili zako kulisoma Neno, Bibilia
Ombi
Endapo wahitaji msaada zaidi, tafadhali wasiliana nasi maana tuko hapa kwa ajili yako. Anwani na nambari ya simu taisoma baada ya wimbo.
WIMBO

Matumaini
TWR
SLP 21514 Code 00505
NAIROBI ,KENYA
Simu/ SMS: 0721 970 520
Barua pepe: [email protected]

Jina langu ni David Mungai.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!