Ukweli Wa Ahadi Ya Ibrahimu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Ukweli Wa Ahadi Ya Ibrahimu
/
Warumi 4:13-18

Hujambo na karibu. Leo twalichabua neno la mungu kutoka warumi 4:13-18, ukweli wa ahadi ya ibrahimu. Jina langu ni David mungai. Karibu wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena. Mtu anatuahidi kitu kila wakati sisi hutarajia kwamba mtu yule atatimiza ahadi yake. Na kweli twafurahia watu kama hao. Mungu wetu ni zaidiwa binadamu maana yeye daima hutimiza kila ahadi anayotuahidi anaweza kukawia lakini hutimiza ahadi zake kwetu. Nasoma sasa fungu la neno kutoka warumi 4:13-18

13 Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani.

14 Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika.

15 Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.

16 Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote;

17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.

18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Ukweli wa ahadi ya ibrahimu ukweli huu umeonyeshwa namna mtume Paulo anaufafanua katika fungu hili la neno la mungu

Kwanza kabisa ahadi imewekwa wazi ahadi kwamba ibrahimu atakuwa mrithi wa dunia ilikamilishwa kwa Imani wala si kwa matendo ya torati au sharia.

Aliamini ya neno la munguzaburi 2:8

Uniombe, nami nitakupa mataifa kwa urithi wako na miisho ya dunia kuwa miliki yako.

Msatari wa 13;

13 Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani.

Kwa kutaja uzao wake ibrahimu kwa maanisha kwa ahadi hii ilikamilishwa kwa kristo maana ndiye aliyeyatimiza maagizo yote ya torati

Historia yote hata miaka 430 ya utumwa nchini misri ilikamilishwa katika kristo kwa sababu kristo ni mungu alikuweko kabla historia b ahata wa leo sisi huhesabiwa kwa kumwamini Yesu kristo

Na ahadi hiyo ni ya pekee kama inavyoelezwa vizuri katika maneno ya mstari wa 15 kwasababu sharia ndiyo ifanyayo hasira maana pasipokuwapo sharia hapana kosa

Hata kama mahakama zetu sharia ndio hutoa hukumu pia katika mambo ya mungu sharia au neno la mungu husema

Ezekieli 18:14

Tazama roho zote ni mali yangu, kama vile roho ya baba ni mali yangu ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu, roho itendayo dhambi itakufalakini kama vile tumesoma katika mstari wa 15 warumi, huruma zake mungu na msamaha wa dhambi na kusamehewa bila sheri, bali kwa Imani

Jambo au ukweli wa tatu, ahadi zake mungu kwa ibrahimu nasi pia ahadi hizo ni kweli, maana mungu milele na milele hutimiza ahadi zake kwetu mstari wa 18

18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Ukweli wa ahadi ya ibrahimu ukweli huu umeonyeshwa namna mtume Paulo anaufafanua katika fungu hili la neno la mungu

Hamna wasiwasi hivyo itakavyo kuwa maana ni mwanyezi amesema na akisema amesema na ndivyoaitakavyo kuwa

Ahadi za mungu hutimizwa kwa neema yake mungu. Ni kwa kumwamini Yesu sio kwa matendo. Matendo huweka muhuri na kudhihirisha wokovu wetu kwatika kristo