Mungu Ni Wa Kwei

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Ni Wa Kwei
Loading
/
Isaya 45:18-23

Hujambo na karibu katika matumaini leo twalichambua neno la mungu kutoka chuo cha nabii isaya 45:18-23 mungu wa kweli. Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naa, karibu tena. Talisoma kwa undani neno lake mungu kutoka chuo cha nabii isaya45:18-23 mungu wetu kweli ndiye mungu wa kweli maana neno lake mungu linasema na kusisitiza hivyo. Nasoma sasa kutoka chuo cha nabii isaya 45:18-25 ili tuwe na amani moyoni na kumpokea na kujitoa kwake mungu maana ndiye mfalme na mpaji wa amani ya kweli na yakudumu.

18 Maana bwana aliyeziumba mbingu na ndiye aliyeimba dunia na kuifanya ndiye aliyeifanya imara hakuiumba ukiwa aliiumba ili ikaliwe na watu. Mimi ni bwana wala hapanna mwingine

19 sikusema kwa siri, katika mahali pa nchi ya gaza sikuwaambia wazao wa Yakobo, nitafuteni bure, mimi, bwana nasema haki nanena mambo ya adili.

20 jikusajyeji mje na kukaribia pamoja nanyi wa mataifa mliookoka, hawana maarifa wale wachukiao mti wa sanamu yao ya kuchonga, wamwombao mumgu asiyeweza kuokoa.

21 Hubirini, toeni habari naam na wafanye mashauri pamoja , ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyehubiri hapo zamani za kale? Si mimi bwana?

22 nianfalieni ,I,I kaokolewe, enyi nchi zote za dunia maana mimi ni ungu hapana mwingine.

23 kwa nafsi yangu, nimeapa neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki walahalitarudi ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa na kila ulimi utaapa.

Katika fungu hili la neno la mungu, Mungu atuonyesha kwamba yeye ni muumbaji mstari wa 18

18 Maana bwana aliyeziumba mbingu na ndiye aliyeimba dunia na kuifanya ndiye aliyeifanya imara hakuiumba ukiwa aliiumba ili ikaliwe na watu. Mimi ni bwana wala hapanna mwingine

Twaona kwamba, mungu ni mkweli kwa sababu twaona uumbaji wake aliumba vyote kwa kusudi na lengo la kutuonyesha kwamba yeye ni mungu

Mungu wa kweli ametufunukia ukweli na kwa hiyo twaweka imani yetu kwake. Hata sisi wanadamu tukimjua mtu wa kwa kweli twaweza kumwamini anaposema jambo au anapotenda jambo.

Kunao watu wanaosema au kufundisha uongo, lakini watamani kuonekana wafaya au watenda kweli. Watu kama hao hawawezi kufunua ukweli.

Kunayo habari ya ukweli. mtu mmoja alikuwa anajifanya kuwa aweza kuwafufua wafu na kumbe ilikuwa ni sarakasi tu. Alimyemelea mmoja wa wale walikuwa karibu naye. Ukweli na usemwe. Akamhonga akamwambia, “tukubaliane nawe, utaingia ndani ya jeneza ujifanye kuwa umekufa na utakaposikia nikisema neonoflani tingiza mwili wako ukiwa ndani yajeniza, na jenezalikifunguliwa uruke nje.

Basi ikawa hivyo. Jamaa akawekwa ndani ya jeneza akaletwa mbele ya halaiki ya watu, aliyetoa hotuba aliirefusha mno Yule jamma jenezani kakakosa hewa ya kutosha akaaga. Alipoitwa kufufuka alikuwa tayari ameaga. Hangeweza kuufuna ukweli.

Mungu si hivy, neno lasema;

21 Hubirini, toeni habari naam na wafanye mashauri pamoja , ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyehubiri hapo zamani za kale? Si mimi bwana?

22 niangalieni mimi ili mkaokolewe, enyi nchi zote za dunia maana mimi ni ungu hapana mwingine.

23 kwa nafsi yangu, nimeapa neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki walahalitarudi ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa na kila ulimi utaapa.

Katika kristo, baba mungu wetu amejifunua kwetu. Katika uumbaji mungu wetu amejifunua kwetu

Mungu aliyatenda yote kwa sabau ndiye mwokozi na mkombozi wetu

22 niangalieni mimi ili mkaokolewe, enyi nchi zote za dunia maana mimi ni ungu hapana mwingine.

Ulimwengu wote naujue kwamba Mungu ndiye aokoaye. Njia I wazi, mungu awaita kila mmoja ampokee moyoni naye atampa wokovu kutika mauti ya milele.

Mungu wa kweli amejifunua na kujidhihirisha kwetu na ni mwokozi na mkombozi wa kila amliliaye na kutubu na kuungama dhambi.twaokolewa kwa neema yake wala si kwa vitendo na kumkirir yesu moyoni.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!