Mungu Ni Wa Ajabu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Ni Wa Ajabu
Loading
/
Isaya 64:1-9

Hujanbo msikilizaji wangu na karibu, leo twalitazama neno kwa undani. Chuo cha nabii Isaya 64:1-9, Mungu wa maajabu . Jina langu ni David Mungai. Furahia wimbo huu alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena. Mungu wetu ni wa maajabu. Mlimani Sinai, mungu kwa mkono wa musa alitoa amri kumi akiwataka watu wake wasimwabudu mungu mwingine wasikajichingee sanamu wakaiabudu akawaambia kitoak 20:1-6

1 Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema,

2 Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri, ambako ulikuwa mtumwa.

3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

4 Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago cha chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia.

5 Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao.

6 Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

Mungu huvutiwa sana na ibada zetu tunapomwabudu kwa roho na kweli. Mungu wetu wa ajabu.

Nasoma sasa kutokachuo cha nabii Isaya 64:1-9

1 Laiti ungepasua mbingu, na kushuka, ili milima iteteme mbele zako;

2 kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, mataifa wakatetemeke mbele zako!

3 Ulipofanya mambo ya kutisha tusiyoyatazamia, ulishuka, milima ikatetema mbele zako.

4 Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye.

5 Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika mambo haya muda mwingi; nasi, je! Tutaokolewa?

6 Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.

7 Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu.

8 Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.

9 Ee Bwana, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.

Kutoka kwa fungu hili la neno la mungu, nabii isaya atatuonyesha maajabu kadhaa ya mungu

Mungu yupo kila mahali ulimwenguni. Na ukweli huu hutuchangamsha tunapojua na kuamini kwamba mungu yu nasi popote pale tulipo na kwa sababu sis tu wenye dgambi kama sivyo kwa huruma zake mungu angetuangamiza ndio sababu nabii Isaya asena ,…laiti ungepasuambingu na kushuka… ni jambo la kustaajabisha kuwa mungu yu kila mahali ulimwenguni na ayaona yote yaliyomo na yasiyo kuwemo.

Hatujasikia wala kuona vile mungu hutupatia riziki zetu za kilasiku. Neno limesema,

4 Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye.

Janbo la tatu, Ingawa sisi ni wenye fhambi na mshahara wa dhambi ni mauti, ni ajabu kwamba mungu yu tayari kushauriana nasi atusamehe dhambi zetu mstari wa 9:

9 Ee Bwana, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.

Ni ajabu kwamba mungu yu pamoja nasi hutupatia riziki za kilasiku na hutusamehe dhambi zetu zote tunapotubu na kuungama dhambi zetu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!