Matumaini ya Leo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Matumaini ya Leo
Loading
/

MATUMAINI PROG. NO. 1482
TITLE: MANENO YA MWISHO
TEXT: 2 CORINTHIANS 12:19-21
Hujambo na karibu tujifunze neon la mungu pamoja. Leo twalichambua fungu la neon kutoka 2 wakorintho 12:19-21, maneno ya mwisho. Jina langu ni David Mungai. Wimbo alafu tuendelee.
WIMBO
Naam karibu tena. Leo twalitazama neon la mungu kwa kina zaid maneno ya Paulo ya mwisho kama yanavyopatikana katika 2 wakorintho 12:19-21 nasoma maneno hayo

19 Je, ninyi mmekuwa mkifikiri muda huu wote kwamba sisi tumekuwa tukijitetea kwenu? Sisi tunasema mbele za Mungu kuhusiana na Kristo. Lakini, wapendwa, mambo yote ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.
20 Kwa maana naogopa kwamba kwa njia fulani, nitakapofika, huenda nikawapata ninyi mkiwa vile ambavyo mimi sipendi nami niwe kwenu vile ambavyo ninyi hampendi, bali, badala yake, kwa njia fulani inaelekea kutakuwa na mizozo, wivu, milipuko ya hasira, magomvi, masengenyo, manong’onezo, majivuno, machafuko.
21 Labda, nitakapokuja tena, huenda Mungu wangu akaninyenyekeza katikati yenu, nami huenda nikaomboleza juu ya wengi kati ya wale ambao hapo zamani walitenda dhambi lakini hawajatubu kutokana na unajisi wao na uasherati na mwenendo mpotovu ambao wamezoea kutenda.

Katika mstari wa 20, baadhi ya maneno yake ni haya
20 Kwa maana naogopa kwamba kwa njia fulani, nitakapofika, huenda nikawapata ninyi mkiwa vile ambavyo mimi sipendi nami niwe kwenu vile ambavyo ninyi hampendi, bali, badala yake, kwa njia fulani inaelekea kutakuwa na mizozo, wivu, milipuko ya hasira, magomvi, masengenyo, manong’onezo, majivuno, machafuko.
Paulo alikuwa anawahofia wakristo kwa sababu licha ya mafundisho mengi bado walikuwa wamejihusihsa na mambo yaliyokinyume na Imani ya kikristo kama vile fitina, wivu, ghadhabu, ugomvi kati yao wenyewe na mengine mengi.
Paulo aliwaombea wakorintho wapate kutubu na kuungama dhambi zile wasije wakahukumiwa kama awali. Hebu msome stari wa tako katika 1 wakorintho 2:5
Wakorintho kama ilivyo hali ya wanadamu walikuwa wanategemea hekima ya kibinadamu walikuwa wanategemea hekima ya kibinadamu, na ingawa si mbaya lakini huzidi hekima kutoka kwa mungu. Paulo alihofia hayo maana yangeweza kuwaingiza katika ibada ya sanamu.
Hakuna mwingine au chombo chochote

Hakuna mwingine awezaye yote au chombo au kitu chochote kinacho weza kufananishwa na hekima kutoka kwa mwenyezi Mungu baba wet una baba wa mwana wetu Yesu Kristo. Hekima ya binadamu ikilinganishwa na Munu ni kama tone la maji ndani ya bahari
Petro alitushauri basi nyenyekeeni chini ya mkono wa mungu ulio hodari naye atawakweza kwa wakati wake.
OMBI
Endapo wahitaji msaada Zaidi tafadhali wasiliana nasi. Anwani na nambari ya simu, ni baada ya wimbo huu
Wimbo
MATUMAINI
TWR,
SLP 21514-00505
NAIROBI KENYA
SIMU: 0721970520
BARUA PEPE: [email protected]
Jina langu ni david mungai, kwaheri

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!