Hatari Ya Kupoteza Nafasi

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Hatari Ya Kupoteza Nafasi
/
Mathayo 23:37-39

Hujambo na karibu tujifunze neno la Mungu pamoja. Leo twalichambua neno kutoka Injili ya Mathayo 23:37-39. Hatari ya kupoteza nafasi. Jina langu ni David Mungai.

Kwa sababu twaishi Maisha ya hekaheka nyingi na changamoto tele, twahitaji kujua namna ya kutumia muda tunaopea na mungu, maana ni mwingi wa huruma na rehema. Ukipata nafasi ya kazi, ukomboe wakati masaa na dakika, kuutumia muda huo kwa njia nzuri makinika bwana upate riziki ya kila siku. Okoa wakati acha kutumia wakati wako ovyo ovyo, usije ukasema, siku za uso kama ningalijua. Okoa wakati siku hizi ni mbaya na zina uovu mwingi.

Mwandishi mmoja shakespare aliandika na kusema, kwa shetani ni patupu, maana uovu umezidi duniani, na siku ya hukumu haijafika. Upatapo nafasi wajibika vilivyo, haujui ya kesho. Usije ukasema ningalijua…hatuwezi kukosoa yaliyopita, lakini twapaswa kujifunza mengi na yaliyopita na twaweza kufanya mengi sasa na tuyafanye vizuri Zaidi.

Nasoma sasa kutoka injili ya mathayo 23:37-39. Yesu awaita watu wake na kuwapa onyo la matokeo ya nafasi walizopoteza. Injili ya mathayo 23:37-39.

Ee, YerusalemuYerusalemu uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake. Lakini hamkutaka! Angalieni nyumba yenu, mmeachiwa hali ya ukiwa. Angalieni, maana nawaaambia hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.

Hapa twamwona Yesu akililia mji wa Yerusalemu-yaani taifa lote la Israeli. Na neno nyumba katika mstari wa 38, azungumza kuhusu viongozi wa kidini mjini Yerusalemu. Anawambia uongozi wote wa kiyahudi utaangamizwa mnamo mwaka wa 70 baada ya kuzaliwa Kristo.

Yerusalemu, ni mahali na mji ambao ungewakaribisha manabii wa mungu, lakini kama vile tumesoma, waliwaka manabii wa mungu. Waliwapiga mawe. Walikaidi maagizo yake mungu na Yesu aliwalilia wale viongozi n ahata mji wenyewe akasema “ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vywake. Chini ya mabawa yake lakini hamkutaka!” kwa huruma nyingi Bwana na Mwokozi Yesu aliwalilia wayahudi. Lakini wakakaidi, wakajifanya kaa ngumu, na kilichofuata ni hukumu. “Angalieni nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa” wakapoteza nafasi ya wokovu na mambo yakaendelea yale ambayo hayakutendeka, na nafasi ikapotea hivyo, ikawa basi ni kungojea hukumu licha ya kuonywa. Mungu ni wa huruma nyingi, hamnyimi mtu nafasi ya kuungama, kabla ya hukumu. Yeye hutupatia nafasi hata ya pili na tatu kabla ya hukumu. Upendo usiokuwa wa kawaida. Angalieni nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.

Ndipo Yesu awaambia, “Kwa maana nawaambianhamtaniona kamwe tangu sasa hata mtakaposema, amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.”

Baadhi ya wenyeji wa Yerusalemu waliwmona Yesu kama mwiba mwilini. Hawakumpenda, na wengine wakashauriana kumwuua. Ndipo akawaambia hamtaniona kamwe tangu sasa lakini akaongezea..hata mtakaposema, amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.

Pengezo kwamba Yesu atarusi tena. Kwa maneno mengine Yesu asema, nawaacha kwa muda lakini mtarudi. Maneno haya aliyanukulu kutoka zaburi ya 118:26 “Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA.”

Anawaambia ya kwamba atawarudia tena. Watakapokiri Yesu ni Bwana, na kuishi nao. Tunapopoteza nafasi, ni onyo kali na kubwa kwetu. Hatuna wakati wa kungojea rafiki yangu. Natufanye tunalopaswa kufanya sasa bila kukawia. Kama ni kumwamini Yesu-ni sasa, acha kupoteza wakati. Kama ni ajira fanya sasa. Hatujui siku ya kurudi Bwana wetu Yesu Kristo, kulinyakua kanisa la wamwaminio.