Kufunika Kichwa – Wanawake Wakristo

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kufunika Kichwa – Wanawake Wakristo
/
I Wakorintho 11:2-16

Natumai u buheri wa afya msikilizaji wangu. Leo twalichambua fungu la Neno kutoka 1 Wakorintho 11:2-16. “Kufunika kwa vichwa wanawake Wakristo.” Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu. “Ufunikaji wa vichwa kwa wanawake Wakristo. Hili jambo ambalo limeshusha utata mno na migawanyoko katika makanisa na shirika nyingi. Lakini Neno lasema na kufundisha aje? Nasoma.

2 Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.

3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.

5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.

6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.

7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.

8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.

9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.

10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.

11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.

12 Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.

13 Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?

14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?

15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.

16 Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.

Hapa twaonyeshwa wazi namna ukweli huu unavyoandaliwa. Mst 2-3 Tuna Mungu wetu Yesu Kristo, tunaye mwanamu na tunaye mwanamke.

Pamoja na hayo tuna uhusiano. Mungu Baba katika mambo yote, Kristo ndiye mkombozi na mpatanishi wet una Mungu. Na uhusiano wa mwanamume na mwanamke ni wazi. Hata maumbile yenyewe yaonyesha wazi. Maneno ya mstari wa 7 yaonyesha ya kwamba. “….”

Na mstari wa 10 waonyesha mamlaka. Yaani, kwa kufunika kichwa huonyesha mamlaka, kwa sababu ya malaika wa Mungu katika ibada kwa sababu ya heshima. Katika chou cha Nabii Isaya 6, twawaona malaika wakijifunika vichwa na nyuso kwa utukufu wa Mungu.

Kwa kifupi ni kwamba, katika hali ya ibada, siyo kilemba, wala chochote kile, twapaswa kutoa heshima zetu, na kila kitu tulicho nacho, kwa utukufu wa Mungu.

Pia ijulikane kuwa nywele ndefu ni utukufu wake mwanamke, lakini isizidi utukufu tunaompa Mungu. Yote tunayotenda ni kwa utukufu wa Bwana Yesu Kristo.

Pamoja na hayo, mavazi yapaswa kuonyesha wote kwamba, mtu ni wa jinsia gani, na yatoa heshima na utukufu kwake Mungu. Kunao dada zutu ambao ukiona vile wamejifunga kitambaa cha kichwa utaona kwamba ni wate…. Wake Mungu kwa huduma maalum.

Kilemba hutuma ujumbe kwa watu wengine kwamba twatamani kuishi tukimtukuza Mungu kwa unyenyekevu, na heshima kati ya wanaume na wanawake nyumbani na Kanisani. Na msingi umewekwa katika Neno lake Mungu. Heshima idumu kati yetu sote Wakristo. Na hayo ndiyo mapenzi yake Mungu.