Watumishi Wa Agano

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Watumishi Wa Agano
/
II Wakorintho 3:1-18

Hujambo. Karibu tulichambue Neno pamoja, kutoka 2 Wakorintho 3:1-18 ‘WATUMISHI WA AGANO’. Jina langu ni David Mungai Karibu. wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena, tujifunze Neno pamoja. 2 Wakorintho 3:1-18. Tutaligawa fungu hili la Neno sehemu mbili (1) Mstari wa 1-3. Pendekezo la huduma. (2) Agano la huduma. Mstari 4-18.

Nasoma, Wakorintho 3:1-18

1 Je, Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine? Barua zenye sitakuja kwenu au kutoka kwenu,

2 Ninyi ndinyi barua yetu iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote

3 mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tulioikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa roho wa Mungu aliye hai. Si katika vibao vya mawe, ila ni katika vibao ambavyo ni moyo ya nyama.”

Kwa kifupi, fungu hili la Neno lafunza kwamba, kazi ya roho mtakatifu maishini mwa mkristo , ni barua Tosha, ya huduma tunayofanya. Mwalimu wa Neno au mhubiri lazima akubali kuongozwa na Roho mtakatifu katika uwajibikaji huduma zetu za kueneza Injili ya wokovu na kuimarika katika imani yetu.

Maisha ya mkristo huongozwa na kuhuishwa na Roho mtakatifu.

AGANO LA HUDUMA: Mstari wa 4-18. “na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo.

5 Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri Neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu.

6 naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya, si wa andiko, bali wa Roho, kwa maana andiko huua bali roho huhuisha.

7 Basi ikawa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata waisraeli hawakuweza kuukazia ,macho uso wa Musa kwa sababu ya utukufu wa uso wake, nao ni utukufu uliokua ukibatilika.

8 Je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu?

9 kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi.

10 maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana

11 kwa maana, ikiwa ile inayobatilika, ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.

12 Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi.

13 nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba waisraeli wasitazame sana, mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika,

14 ila fikira zao zilitiwa uzito, kwa maana hata leo hivi, wakati liswomapo Agano la kale, utaji uo huo wakaa, yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo.

15 ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.

16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

17 Basi, Bwana ndiye Roho, walakini alipo Roho wa Bwana hapo ndipo penye nuru.

18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano huo, toka utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

Agano jipya hili, ni Ujumbe wa neema kwake Yesu Kristo.

Kama tulivyosoma katika Mstari 6 “…andiko huua bali roho huhuisha..” Andiko yaani Torati pekee, haingeleta wokovu na ondoleo ya dhambi, Lakini Yesu Kristo huhuisha kwa sababu ndiye pekee aliweza kuyakamilisha kwa kifo chake cha msalaba. Roho mtakatifu wa Mungu humuhuisha, anayemwamini Yesu Kristo. Na kama tunavyosoma katika mstari wa 18.“Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano huo, toka utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.”

Torati ni mwalimu wa kutuonyesha vile hatuwezi kujiokoa kwa matendo yetu. Ukiweka tisa na ukosee moja una hatia ya zote na hukumu yake ni kifo katika moto uwakao kiberiti. Bwana wetu Yesu, hakuvunja sheria hata moja kwa hiyo, alikufa, alisulubiwa kwa niaba na kwa ajili yetu, ili tukimwamini tusamehewe dhambi na kuokolewa, na hatimaye tupate utukufu hata utukufu.