Wakati Ndoto Hutegemewa

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Wakati Ndoto Hutegemewa
Loading
/
Mwanzo 40:1-23

Hujambo na karibu. Leo katika matumaini tutajifunza namna na wakati ndoto zaweza kutegemewa. Somo letu ni kutoka Mwanzo 40:1-23. Jina langu ni david mungai. Katika Maisha yetu huishi na matarajio. Watu wengine husema kwamba wapewa uwezo kutoka kwa mungu, kuwaambia mambo yao yayao, kwa kutumia mbinu na njia nyingi.

Kunazo nyakat ambamo ndoto zimetegemewa sana. Kunao watu wameongozwa na mwenyezi mungu kwa ndoto. Shetani pia aweza kutumia ndoto zetu, za uongo na kuangamiza. Tumejifunza kutoka kwa ndoto za yusufu vile alidhauriwa na ndugu zake. Yusufu alipowekwa jela, twaona vile alitafsiri ndoto za wafungwa wengine. Nasoma kutoka mwanzo 40:1-23

Ikawa baada ya mambo hayo mnyweshaji wa mfalme wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa misri. Farao akawaghadhibikia maakida wake wawili, mkuu wa waokaji. Akawatia katika lindo nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani mahali alipofungwa yusufu.

Mkuu wa askari akamweka yusufu watu hao, naye akawahudumu nao wakakaa siku kadha wa kadha katika kifungo. Wakaota ndoto wote wawili kila mtu ndoto yake usiku. Mmoja kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa misir waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi akawaona wamefadhaika.

Akawauliza hao maakida wa farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo nyumbani mwa bwana wake, akisema mbona nyuso zenu zimekunjanama leo? Wakamwambia tumeota ndoto wala hapana awezaye kutafsiri yusufu akawaambia, kufasiri si kazi ya mungu? Tafadhalini mniambie. Mnyweshaji mkuu akamhadithia yusufu yake. Akamwambia katika ndoto yangu nimeota uko mzabibu mbele yangu. N akatika mzabibu mlikuwa na matawi matatu nao ulikuwa kana unamea unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiwa. Na kikombe cha farao kilikuwa mkononi mwangu nikazitwaa zabibu nikazikamua katika kikombe cha farao nikampa farao kikombe mkononi mwake.

Yusufu akamwambia. Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. Baada ya siku tatu farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako, nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake kama desturi ya kwanza ulipokuwa mnyweshaji wake. Kwa sababu hakika naliibiwa kutoka nchi ya waebrania wala hapa sikutenda neno lo lote hata wanitie gerezani. Mkuu wa waokoji alipona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema akamwambia yusufu. Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu na tazama ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa change. Na katika ungo wa juu mlikuwa na kila namna ya chakula kwa farao kazi za mwokaji ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.

Yusufu akajibu akasema. Tafsiri yake ndiyo hii, nyundo tatu ni siku tatu. Baada ya siku tatu farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako. Ikawa siku ya tatu siku ya kuzaliwa kwake farao akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji na cha mkuu wa waokaji miongoni mwa wa watumwa wake. Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha naye akampa farao kikombe mkononi mwake. Basi akamtundika mkuu wa waokaji kama yusufu alivyowafasiria. Lakini huyo mkuu wa wanyweshaji hakumbuka yusufu alimsahau.

Je hapa twaweza kujifunza mambo matatu. Mungu aweza kutumia ndoto za kawaida kwa njia ya kipekee. Ndoto ni za kawaida na watu ni wa kawaida. Mungu aliweza kutumia ndoto zao, kuwazungumzia.

Funzo la pili. Kama alivyofanya yusufu ni mcha mung utu aweza kutafsiri ndoto. Kama si yusufu wanaume hao wawili hawangejua maana ya ndoto zao. Yusufu alimcha mungu. Funzo la tatu. Siyo kila ndoto huwa na maana kubwa siku zetu hazitili maanani ndoto sana kwa sababu mungu amejifunua mwenyewe na mapenzi yake kwetu katika biblia biblia ndiyo humwongoza mkristo na kuyapata mapenzi yake mungu katika biblia yake mungu katika biblia basi ni heri na ni muhimu kulisoma neno lake mungu na kulitafakari na kulitii katika kuzingatia mapenzi ya mungu yaliyo sahihi.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!